Ulimwengu wa Michezo

Ulimwengu wa Michezo

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Ulimwengu wa Michezo, Public Figure, sinoni, Arusha.

https://www.instagram.com/shabanifundisports?igsh=MTZlcnBhNzhoNGJqZQ==

MICHEZO ZAIDI @YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB NA SIMBA SC TANZANIA

KARIBUNI SANA

hatufungamani na timu yoyote Ile usiache kunifollow kwa update zote

26/09/2026

๐ŸŒ… ASUBUHI NJEMA WANANCHI! ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

Kila mmoja anayeiona asubuhi hii, tunamtakia siku yenye amani, afya, baraka na mafanikio. ๐Ÿคฒ๐Ÿฝ

Kila jambo jema unalolipangia leo, Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi na akufungulie milango ya riziki na mafanikio. โค๏ธ

Anza siku kwa tabasamu, moyo wa shukrani na matumaini mapya.
Usikate tamaaโ€”huenda leo ndiyo siku ambayo ulikuwa ukiisubiri. ๐Ÿ’ช๐Ÿฝ

โ˜€๏ธ ASUBUHI NJEMA WANANCHI WOTE!

Ulimwengu wa Michezo Sauti ya Wananchi

25/09/2026

Nakuja na nondo

Silazi damu. Ulimwengu wa Michezo

22/09/2026

๐ŸŽ‰๐ŸŽ‚ HAPPY BIRTHDAY, CHEIKH TOURร‰ IBRAHIM! ๐Ÿ’š๐Ÿ’›

Ulimwengu wa Michezo

Tunakupongeza na kukutakia heri ya siku yako ya kuzaliwa . ๐Ÿคฒ๐Ÿฝ

Mungu akuongezee afya, nguvu, furaha na mafanikio zaidi katika maisha yako na ndani ya familia ya Young Africans Sports Club . ๐Ÿ’š๐Ÿ’›

Happy Birthday, Champion! ๐Ÿฅณ๐Ÿ”ฅ

Photos from Ulimwengu wa Michezo's post 22/09/2026

KABLA YA JINA, KULIKUWA NA SAFARIโ€ฆ

Kabla dunia haijalifahamu jina la SHABANI FUNDI SPORTS, kulikuwa na kijiji kidogo, kulikuwa na madawati ya shule, kulikuwa na walimu, kulikuwa na malezi, kulikuwa na maonyo, kulikuwa na ndoto โ€” na kulikuwa na mtoto aliyekuwa akijifunza hatua kwa hatua namna ya kuifahamu dunia.

Kila jina lenye uzito huwa na historia iliyojificha nyuma yake. Na kila hatua inayodhihirika leo huwa imechipuka kutoka kwenye mizizi iliyowahi kumwagiliwa kwa jasho, mafunzo, nidhamu na uvumilivu.

Mimi ni SHABANi HALIDI MBAYA , mzaliwa na mlezi wa Kijiji cha Kwakombo, Kata ya Kwamsisi, Wilaya ya Korogwe โ€” mahali ambapo safari yangu ilipata mwanzo wake, na ambako misingi ya utu, heshima na elimu ilianza kuchongwa ndani yangu.

Nilianzia safari yangu ya elimu katika Shule ya Msingi Kwakombo. Hapo ndipo nilipokutana na walimu ambao leo, nikitazama nyuma kwa jicho la kumbukumbu, naona hawakuwa wakifundisha masomo pekee; walikuwa wakijenga mwanadamu.

Miongoni mwao walikuwapo Mwalimu Idd Machaku, Mwalimu Mgaza na Mwalimu Antazi Mtenga.

Na kwa heshima isiyopimika kwa maneno, jina la Mwalimu Idd Machaku linachukua nafasi ya pekee katika historia yangu.

Alikuwa zaidi ya mwalimu. Alikuwa nguzo katika ujenzi wa misingi ya heshima, nidhamu na utu. Mafundisho yake hayakuishia kwenye ubao wa darasa wala kurasa za madaftari; baadhi yake yalipenya ndani ya maisha na kubaki kuwa sehemu ya mwenendo wangu.

Mwalimu wangu Idd Machaku, Mwenyezi Mungu akujalie afya njema, akulinde, akupe nguvu na akurefushe umri wako katika kheri na baraka. ๐Ÿคฒ๐Ÿฝ

Baada ya hapo, upepo wa safari ya elimu ukanifikisha Shule ya Sekondari Joel Bendera, ambako niliendelea kusukwa na maarifa na malezi.

Huko nikakutana na walimu waliokuwa sehemu ya ukurasa mwingine wa maisha yangu; akiwamo Mwalimu Mkuu Msemwa pamoja na Madam Lightness.

Katika somo la Kiswahili, nilipata bahati ya kufundishwa na Mwalimu Dunia, huku katika Historia nikiongozwa na Mwalimu Semango.

Leo ninapotazama nilikotoka, ninatambua kwamba hakuna mwanafunzi anayejijenga kwa mikono yake mwenyewe pekee.

Nyuma ya kila hatua kuna mwalimu aliyewahi kusimama mbele ya darasa, mzazi aliyewahi kutoa jasho, mlezi aliyewahi kutoa nasaha, na jamii iliyowahi kumlea mtoto huyo bila kujua siku moja angekuwa nani.

Kwa hiyo, SHABANI FUNDI SPORTS si jina lililodondoka kutoka angani.

Ndani yake kuna Kwakombo. Kuna Kwamsisi. Kuna Korogwe. Kuna madawati ya shule. Kuna vitabu. Kuna walimu. Kuna maonyo. Kuna nidhamu. Kuna heshima. Kuna ndoto za mtoto wa jana ambazo leo zimeanza kupata sura.

Kwa walimu wangu wote walionifundisha, kuniongoza, kunikosoa, kunitia moyo na kuniamini:

Ninawapa heshima yangu ya dhati.

Huenda siku zile sikuwa na uwezo wa kutambua thamani ya kila neno mliloniambia; lakini leo, kila ninapopiga hatua, ninaiona thamani ya yale mliyopanda ndani yangu.

Najivunia kuwa mwanafunzi wenu.
Najivunia mizizi yangu.
Najivunia nilikotoka.
Na zaidi ya yote, najivunia kuwa sehemu ya kizazi kilicholelewa na walimu wenye moyo wa kufundisha na kulea.

Kutoka Kwakombo hadi kwenye jukwaa la michezo.

Kutoka madawati ya shule hadi kwenye kalamu ya uandishi.

Kutoka kwa mwanafunzi wa jana hadi kuwa SHABANI FUNDI SPORTS wa leo.

Hii si historia ya jina pekee; ni historia ya malezi, elimu, walimu, heshima, nidhamu na safari isiyokatika ya maisha.

Ulimwengu wa Michezo

Sauti ya Wananchi.
Ukweli na Uwazi.
Heshima kwa nilikotoka, fahari kwa nilipo, na matumaini kwa ninakokwenda.

22/09/2026

๐Ÿšจ ๐๐‘๐„๐€๐Š๐ˆ๐๐† | ๐‚๐„๐ƒ๐‘๐ˆ๐‚ ๐Š๐€๐™๐„ ๐๐ˆ ๐Š๐Ž๐‚๐‡๐€ ๐Œ๐๐˜๐€ ๐Š๐€๐†๐„๐‘๐€ ๐’๐”๐†๐€๐‘! ๐Ÿ”ฅ

Cedric Kaze ameteuliwa kuwa Kocha Mkuu mpya wa Kagera Sugar, akichukua nafasi ya Juma Kaseja ambaye ameondolewa pamoja na benchi lake la ufundi. ๐ŸŸขโšฝ

Kaze sasa anapewa jukumu la kuiongoza Kagera Sugar katika safari ya msimu huu, huku macho ya mashabiki yakisubiri kuona mabadiliko yatakayokuja chini ya uongozi wake. ๐Ÿ‘€๐Ÿ”ฅ

๐‚๐„๐ƒ๐‘๐ˆ๐‚ ๐Š๐€๐™๐„ โžก๏ธ ๐Š๐€๐†๐„๐‘๐€ ๐’๐”๐†๐€๐‘

22/09/2026

UONGOZI wa Young Africans Sports Club umepokea kwa huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Mjumbe wa Baraza letu la Wadhamini, Mama Fatma Karume kilichotokea jana, Septemba 21, 2026.

"Huu ni msiba mkubwa kwetu. Tumepoteza Kiongozi mkubwa mwenye busara, hekima na mapenzi makubwa na Klabu yetu. Tutamkumbuka Mama yetu Fatma Karume kwa mengi mazuri aliyofanya ndani ya Klabu yetu ikiwemo upatikanaji wa Ardhi ya jengo letu la Makao Makuu, Jangwani Jijini Dar Es Salaam. Hakika, tumempoteza Mwanachama na moja ya nembo ya Klabu hii," Rais wa YANGA, Eng. Hersi Said.

Uongozi wa YANGA unatoa pole kwa Familia, ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na Wadau wote wa michezo nchini pia tunawaombea wote kwa Mwenyezi Mungu wapate nguvu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Ameen.

Imetolewa na:

Idara ya Habari na Mawasiliano

Young Africans Sports Club

22/09/2026

๐Ÿšจ FEISAL SALUM NA UJUMBE WAKE KWA AZAM! ๐Ÿ‘€๐Ÿ”ฅ

Feisal Salum ameuanza msimu huu akiwa k**a โ€œwa baridiโ€, lakini kwangu hilo halimaanishi moja kwa moja kwamba kiwango chake kimeshuka. Kuna namna fulani ya mambo yanavyoendelea ambayo inanifanya nione k**a huenda kuna ujumbe anautuma kuelekea Azam FC. ๐Ÿ‘€

Inawezekana kabisa suala kubwa likawa ni mkataba mpya na maslahi yake. K**a kile anachokihitaji hakitazingatiwa, huenda siku zake za kuendelea kubaki ndani ya klabu zikawa zinahesabika.

Kuna kauli yake moja kwenye mahojiano ya hivi karibuni ilinifanya nitafakari zaidi. Feisal alieleza kwa msisitizo kuhusu suala la mapenzi kwa timu na kile anachokitafuta kwenye sokaโ€”maslahi yake ya kifedha. ๐Ÿ’ฐ

Sasa hapa ndipo penye mtego wa Feisal kwa Azam. ๐Ÿชค

K**a kweli anataka mkataba wenye thamani kubwa zaidi, basi Azam wanaweza kujikuta kwenye wakati mgumu: ama watoboke na kumlipa kiasi anachokitaka, au waanze kukabiliana na uwezekano wa kumpoteza.

Lakini swali linabaki mojaโ€ฆ

๐Ÿ”ฅ AZAM WATALEGEZA MIKANDA KWA AJILI YA FEISAL, AU HATMA YAKE KLABUNI ITAFIKA MWISHO?

Muda utasema. ๐Ÿ‘€

21/09/2026

๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ’š WACHEZAJI WETU, TAIFA KWANZA! ๐Ÿ”ฐ

Hawa ndio Wachezaji wetu wa Young Africans Sports Club walioitwa kuwakilisha Taifa katika vikosi vya:

๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ TAIFA STARS
๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ U-23
๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ U-20

Ni heshima kubwa kwa klabu na fahari kwa Wananchi kuona vipaji vyetu vikipeperusha bendera ya Tanzania. ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ”ฅ

Nendeni mkaitangaze YANGA, mkaitangaze TANZANIA! ๐Ÿ’š๐Ÿ’›

Ulimwengu wa Michezo

20/09/2026

๐Ÿšฉ ๐…๐”๐‹๐‹ ๐“๐ˆ๐Œ๐„ : Premier League ๐Ÿด๓ ง๓ ข๓ ฅ๓ ฎ๓ ง๓ ฟ

MANCHESTER CITY 5๏ธโƒฃโž–๏ธ3๏ธโƒฃ SUNDERLAND AFC
โšฝ๏ธ 09" Fernandes โšฝ๏ธ 12" Brobbey
โšฝ๏ธ 29" Rayan Cherki โšฝ๏ธ 33" Brobbey
โšฝ๏ธ 43" Semenyo โšฝ๏ธ 59" Brobbey
โšฝ๏ธ 57" Semenyo
โšฝ๏ธ 82" Haaland

Bama โœ๏ธ

20/09/2026

Kapona ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ

Ulimwengu wa Michezo

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Address

Sinoni
Arusha