TMDA
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from TMDA, Government Organization, Dodoma.
21/09/2026
TMDA wahimiza wataalam wa afya Kibaha kuzingatia maadili ktk kusimamia dawa tiba zenye asili ya kulevya ili dawa hizo zisiingie mtaani kinyume na sheria, hayo yamejiri wakati wa mafunzo yaliyotolewa kwa wataalam wa afya wanaosimamia mnyororo wa dawa tarehe 18/09/2026.
20/09/2026
Mnamo tarehe 19 Septemba 2026, TMDA ilitembelea Kiwanda cha MSD cha Uzalishaji wa Glovu, Idofi, Njombe, kutoa mwongozo wa kiudhibiti ili kuhakikisha uzalishaji wa glovu salama na zenye ubora, kwa ajili ya kulinda afya na usalama wa jamii.
20/09/2026
Baraza la Saba la Wafanyakazi wa TMDA lapatiwa mafunzo ya kuimarisha uwajibikaji na ufanisi katika kutekeleza majukumu ya udhibiti na kulinda afya ya jamii. Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 16 Septemba 2026, Iringa.
19/09/2026
16/09/2026
Wakurugenzi na Mameneja wapatiwa mafunzo ya GIAMIS tarehe 15 Septemba 2026, Iringa, kwa lengo la kuimarisha uwajibikaji na ufanisi katika udhibiti wa mifumo na utekelezaji wa majukumu ya kulinda afya ya jamii.
16/09/2026
10/09/2026
HABARILEO with .repost
・・・
DAR ES SALAAM; MAMLAKA ya Dawa na Vifaatiba (TMDA) imesema itateketeza dawa na vifaatiba vyenye thamani ya Sh milioni 300 vilivyokamatwa Septemba 7 na 9, mwaka huu mkoani Dar es Salaam.
-
Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dk Adam Fimbo alisema kushirikiana na Jeshi la Polisi ilibaini uingizaji haramu wa shehena ya dawa kupitia Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) zilitoka nchini India na zikiwa zimehifadhiwa katika masanduku 20.
-
““Dawa hizo hazijasajiliwa nchini hivyo ubora, usalama na ufanisi wake haukuwa umethibitishwa na TMDA.
-
“Hatua ya kuteketeza inalenga kulinda afya za wananchi dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na matumizi ya dawa ambazo ubora, usalama na ufanisi wake haujathibitishwa na mamlaka,” amesema.
-
Amesema Septemba 9, 2026, TMDA ilibaini shehena nyingine iliyokuwa na dawa za sindano, zikiwemo lignokeni, bupivakeni, adrenalini na vitamini.
-
“Uchunguzi wa awali ulionesha kuwa shehena hiyo ilikuwa na viambata hai vinavyotumika katika dawa za kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani, kifafa, shinikizo la juu la damu na kisukari, pamoja na dawa zinazotumika katika kupunguza unene. Pia kulikuwa na vifaatiba vya meno bandia,” alisema Dk Fimbo.
-
Alisema TMDA itaendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kubaini na kuwachukulia hatua wahusika wa uingizaji na biashara ya bidhaa tiba kinyume cha sheria.
-
Dk Fimbo alisema TMDA imeimarisha mifumo ya ukaguzi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuongeza ukaguzi wa kushtukiza katika mipaka, viwanja vya ndege na bandarini, pamoja na kutumia vifaa vya kisasa kupima ubora wa bidhaa tiba.
-
Zaidi tembelea //www.habarileo.co.tz
Imeandaliwa na Aveline Kitomary
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
1253