Iringa Recovery Community - IRC

Iringa Recovery Community - IRC

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Iringa Recovery Community - IRC, Non-Governmental Organization (NGO), Iringa.

A community-based organization supporting individuals and families affected by addiction through recovery services, awareness, and empowerment.
๐Ÿ“ Based in Iringa, Tanzania

11/09/2026

Credits: ๐Ÿ“ฝ NURU FM TZ

10/09/2026

Pombe huathiri kwa kupunguza utendaji kazi (uwezo) wa ubongo wako wa mbele. Ubongo wako wa mbele ndio hukusaidia kufikiri, kufanya maamuzi sahihi, na uwezo wa kupanga mipango.

Jukumu la kuitunza na kuijali afya yako ya mwili na akili ni la kwako si mtu mwingine.

Credits: ๐Ÿ“ฝ Daniel G. Amen, M.D.

10/09/2026

๐Ÿซ‚ Wakati mwingine, maumivu tusiyoyaona ndiyo yanayohitaji uwepo wetu zaidi.

Leo, 10 Septemba โ€” World Su***de Prevention Day, Iringa Recovery Community (IRC) inakumbusha umuhimu wa kutokunyamazia maumivu, kuzungumza, kusikiliza, na kuokoa maisha yetu wenyewe na watu wengine wanaopitia changamoto za kihisia au afya ya akili.

๐Ÿง  Usipuuze mabadiliko ya tabia.
๐Ÿค Usihukumu maumivu ya mwingine.
๐Ÿ’ฌ Uliza. Sikiliza. Kuwa pamoja naye.

Mazungumzo yanaweza kuwa mwanzo wa matumaini.

***dePreventionDay ***dePrevention

Photos from Iringa Recovery Community - IRC's post 09/09/2026

๐ŸŽ™๏ธ USHIRIKI WA VIJANA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

Leo, 09 Septemba 2026, Iringa Recovery Community (IRC) kupitia Mkurugenzi Mtendaji, Ndugu Wilbert Mpanda, ilishiriki katika kipindi cha Nuru FM, pamoja na Afisa kutoka DCEA, Bi. Queen Komba, na Manager wa Iringa Sober House.

Mazungumzo yalilenga kujadili nafasi na umuhimu wa vijana kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya matumizi na usambazaji wa dawa za kulevya, pamoja na namna jamii inavyoweza kuwawezesha vijana kufanya maamuzi salama na kujenga maisha yenye mwelekeo chanya. ๐Ÿง ๐ŸŒฑ

๐Ÿค Mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanahitaji ushirikiano wa kila mmojaโ€”na vijana si watazamaji, ni sehemu muhimu ya suluhisho.



dcea

07/09/2026

๐Ÿง  Usibebe Maumivu Pekee Yako.

Wakati mwingine tunatabasamu mbele za watu, huku ndani tukipitia maumivu ambayo hatujui namna ya kuyaeleza.

Msongo wa mawazo, huzuni, hofu au maumivu ya kihisia yanaweza kuathiri maisha yetu. Huhitaji kupitia kila kitu peke yako. ๐Ÿค

IRC inatoa ushauri nasaha na msaada wa kisaikolojia kwa wanaohitaji nafasi salama ya kuzungumza, kueleweka na kupata mwongozo.

๐ŸŒฑ Kutafuta msaada si udhaifu. Ni hatua ya kujijali.

๐Ÿ“ฒ Kwa mawasiliano, angalia namba iliyopo kwenye Bio yetu.

Photos from Iringa Recovery Community - IRC's post 07/09/2026

87 kati ya watu 100 wenye changamoto kubwa ya matumizi ya pombe hawajawahi kutafuta msaada โ€” hata mara moja.

Sio kwa sababu hawana tatizo. Mara nyingi, aibu, unyanyapaa, kutokujua pa kupata msaada, au imani ya โ€œnitaweza kujishughulikia mwenyeweโ€ huwafanya watu wakae kimya na kuendelea kubeba changamoto zao peke yao. ๐Ÿ’›

Utafiti kutoka Ethiopia unaonyesha jambo muhimu: unyanyapaa hauathiri tu jinsi wengine wanavyomtazama mtu mwenye changamoto ya matumizi ya pombe โ€” unaweza pia kumfanya mtu ajizuie mwenyewe kutafuta msaada anaostahili.

Tunahitaji kubadilisha mtazamo huu. Kujitokeza kuomba msaada si udhaifu. Ni hatua ya kwanza kuelekea kupata nafuu. Tuanze kubadilika, kuanzia na sisi wenyewe. ๐Ÿ’™

Photos from Iringa Recovery Community - IRC's post 06/09/2026

๐Ÿง  Elimu, Uelewa na Ushirikiano kwa Jamii yenye Afya

IRC kupitia Mwanasaikolojia John John Psychologist JOHN JOHN ilipata fursa ya kushiriki katika semina ya siku mbili iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Mtwivila, Iringa, iliyolenga kujenga uelewa kuhusu masuala mbalimbali yanayogusa afya, familia na ustawi wa jamii.

Katika semina hiyo, kupitia wataalamu wake, IRC ilitoa elimu kuhusu maumivu ya kisaikolojia na afya ya akili, madhara ya matumizi ya dawa za kulevya, pamoja na kujitambua na kujenga mahusiano yenye afya.

Pamoja na wadau wengine, tulijadili pia masuala ya ndoa na familia, mwanaume na mwanamke wa thamani, ulinzi na usalama, ukatili, pamoja na afya ya mwili wa binadamu.

Semina hii ilifanyika kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali, wakiwemo Polisi Kata, Mwenyekiti wa Wanaume Jonas Mbass, pamoja na Mratibu wa Afya kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bi. Illuminata Sanga.

๐Ÿค Kwa IRC, tunaamini kuwa jamii yenye uelewa ni jamii yenye uwezo wa kujilinda, kutafuta msaada mapema na kujenga maisha yenye afya. Ndiyo maana tunaendelea kushirikiana na taasisi za dini, Serikali na wadau wengine katika kutoa elimu kuhusu afya ya akili, matumizi ya dawa za kulevya na ustawi wa jamii.

๐ŸŒฑ Tunajenga uelewa. Tunatoa msaada. Tunakuza matumaini.

๐Ÿ“ž Kwa msaada kuhusu huduma za Sober House:
0652 224 459 | 0629 560 327 | 0743 338 512

06/09/2026

Mkurugenzi Mtendaji wetu, Ndg. Wilbert Mpanda, akipokea cheti baada ya kukamilisha mafunzo ya kitaifa ya siku tatu kuhusu usimamizi wa tatizo la matumizi ya pombe kwa kutumia tiba ya Naltrexone โ€” Midland Hotel, Dodoma, 2โ€“4 Septemba 2026.

Cheti kimekabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe.

Tunaishukuru Taasisi ya Afya ya Akili Tanzania (TMHI) kwa mafunzo haya. Ujuzi tulioupata unarudi moja kwa moja kwa wateja wetu wa HATUA Sober House.

01/06/2026
Want your organization to be the top-listed Non Profit Organization in Iringa?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Website

Address

Iringa

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Iringa Recovery Community - IRC posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Subscribe

We will notify you when anything happens in Iringa.