Nuru ya Ulimwengu
NURU YA ULIMWENGU | Light of the World Mission Experience🌍
Equipping believers for cross-cultural evangelism. Bridging faith, culture & mission.🙏🏿
“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;”
— Yohana 1:12
Evangelism.
Warumi 6
³ Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?
⁴ Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi k**a Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
26/09/2026
“Na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua; na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote.”
— Matendo ya Mitume 3:16
25/09/2026
Moshi Evangelism public meeting.
ya Uinjilisti Moshi.
Mathayo 8
⁵ Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia,
⁶ akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.
⁷ Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye.
⁸ Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.
⁹ Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.
¹⁰ Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli. ya Ulimwengu
25/05/2026
KUACHILIA KUNAUMA… LAKINI WAKATI MWINGINE NDIO MAPENZI YA MUNGU
Kuna nyakati katika maisha Mungu huruhusu watu, mazingira au misimu fulani kuingia katika maisha yetu kwa kusudi maalum. Wengine huja kutufundisha, kutuonya, kutujenga au kutuandaa kwa hatua nyingine ya maisha. Lakini tatizo kubwa huwa pale tunapong’ang’ania vitu ambavyo Mungu tayari ameruhusu viondoke.
Wakati mwingine tunaendelea kushikilia mahusiano yasiyo na amani, mazoea mabaya au maisha ya zamani ambayo hayana tena kusudi katika safari yetu ya kiroho. Tunafanya hivyo kwa sababu tunaogopa maumivu ya kuachilia.
Biblia inasema:
“Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.”
— 2 Wakorintho 5:17
Mungu hawezi kutupeleka katika maisha mapya ikiwa bado tumeushikilia kabisa ulimwengu wa zamani. Wakati mwingine uponyaji huanza pale tunapokubali kuachilia.
Biblia pia inasema:
“Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;”
— Wafilipi 3:13
Mtume Paulo alielewa kuwa ili kusonga mbele ni lazima kuacha yaliyopita. Huwezi kuendelea mbele kiroho huku moyo wako umefungwa na maumivu, watu au kumbukumbu za zamani.
Kuna watu Mungu aliwaondoa kwenye maisha yetu sio kutuumiza bali KUTULINDA. Kuna milango iliyofungwa sio kwa sababu Mungu ametuacha bali kwa sababu anaandaa mlango bora zaidi.
“Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.”
— Warumi 8:28
Usiogope kuanza upya pale Mungu anapofunga ukurasa fulani wa maisha yako. Wakati mwingine BARAKA kubwa sio kupata kile unachotaka, bali kupata NGUVU YA KUACHILIA kile ambacho sio mapenzi ya Mungu tena katika maisha yako.
Mungu akubariki.
NuruYaUlimwengu
Nuru ya Ulimwengu . Mafundisho ya Biblia.
Nuru ya Ulimwengu
102.7.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Moshi
Alerts
Be the first to know and let us send you an email when Nuru ya Ulimwengu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.