MTEULETHEBEST.COM

MTEULETHEBEST.COM

Share

Michezo, Siasa , Mitindo ya Maisha na Utani & Vichekesho Ukurasa huu hupo kwa misingi ya burudani na siasa na michezo yote upo kwa kumpafuraha msomaji wake

13/03/2026

Wairani waimba kilipiza kisasi huku bendera ikiwa na damu ya mwanamke aliyeripotiwa kuuawa katika shambulio la bomu la Marekani-Israeli kwenye Siku ya Quds. Maandamano ya Siku ya Quds yameinuliwa juu ya umati.

02/03/2026

❗️TAZAMA: Amri Kuu ya Marekani yatoa video MPYA ya MASHAMBULIZI dhidi ya Iran, na kuharibu kile kinachoonekana kuwa vifyatuaji makombora vya Iran

KARIBU JIUNGE KWENYE GROUP ZA KILINGENI ZA WhatsApp na Telegram

Telegram +255 682033019
https://t.me/KilingeniNews

WhatsApp +255682033019

https://chat.whatsapp.com/K8egtL1TdgN7M7UVtwpZAT?mode=gi_t

NDG. MTEULE GOSBERTH KAHANGILE – WhatsApp channel 30/01/2026

ALIPINDULIWA KWA KUKATA MIRIJA YA MABEBERU IRAN.

Dkt. Mohammad Mossadegh alikuwa Waziri Mkuu wa Iran, aliyechaguliwa na Bunge la 16 la Iran (16th Majlis) mwaka 1951.

Anakumbukwa kwa kutaifisha sekta ya mafuta ya Iran ili kujenga uchumi imara wa taifa na watu wake. Hatua hiyo, iliwaudhi mabepari wa Magharibi. Mirija ya Uingereza na Marekani ilikaushwa na kuzua hasira kubwa kwa makampuni vigogo vya uchimbaji na uchakataji mafuta ya nchi hizo.

Agosti 19, 1953, mapinduzi ya kumuondoa madarakani Mosaddegh yanafanikiwa. Mashirika ya Ujasusi, CIA ya Marekani na MI6 ya Uingereza yalikiri baadae kuhusika na mapinduzi hayo.

Nafasi ya Mossadegh anaichukua Jenerali Fazlollah Zahedi aliyependekezwa na MI6 ili kulinda maslahi ya wakubwa wa Magharibi. Mapinduzi hayo yaliimarisha zaidi utawala wa Reza Shah wa Iran.

Baada ya Mapinduzi, Mossadegh alik**atwa, akatupwa gerezani kwa miaka mitatu, kisha akahukumiwa kifungo cha maisha cha nyumbani, hadi alipofariki dunia mwaka Machi 05,1967 kwa ugonjwa wa saratani na vidonda vya tumbo vilivyochachamaa na kuanza kuvuja damu ndani kwa ndani.

Utawala wa Shah ulikataa kumzika licha ya ombi lake la kuzikwa kwenye makaburi ya umma pembeni ya waathirika wa vurugu za kisiasa waliouawa mwaka 1952.

Ili kuepusha taabu na wenye nchi, familia ilimzika sebuleni kwake. Hadithi ya mwanamageuzi, mwanasiasa aliyetishia umaarufu wa Shah, Mtunzi wa Vitabu na Mwanasheria nguli ikazikwa kwa namna ya fedheha kabisa.

Kupinduliwa kwa serikali ya kidemokrasia iliyotikisa meza ya vinywaji vya gharama vya Magharibi kumeacha alama isiyofutika kwa historia ya Iran, kiasi Waajemi wengi hawana imani kabisa kwa madola ya Magharibi yanayohubiri demokrasia na utawala bora na haki za binadamu, yakiwapaka mafuta mataifa mengi kwa mgongo wa chupa.

Dkt. Mossadegh alizaliwa Juni 16, 1882 na kufariki dunia Machi 05, 1967 akiwa na umri wa miaka 84. Aliacha Watoto watano.

Fuatilia kituo cha KILINGENI kwenye WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VbBK1DyAInPleGrQw71X

NDG. MTEULE GOSBERTH KAHANGILE – WhatsApp channel Follow NDG. MTEULE GOSBERTH KAHANGILE's WhatsApp channel. Kituo hiki kimeundwa mahususi kukuletea taarifa sahihi na za haraka kuhusu Soka, Teknolojia, Biashara, Habari za Kimataifa]. Lengo letu ni kukupa maarifa, habari, na vidokezo muhimu moja kwa moja kwenye simu yako. Jiunge nasi na uwe wa kwanza kujua kinachoendelea!. Join 141 followers for the latest updates.

29/01/2026

Ndege moja aina ya Airbus A321-231 inayomilikiwa na kampuni ya ndege ya Meraj, iliyosajiliwa k**a IRAN07, ambayo kwa kawaida hutumiwa na viongozi wakuu wa utawala wa Kiislamu, iliondoka Tehran kuelekea Moscow, Urusi, mapema leo

Fuatilia kituo cha KILINGENI kwenye WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VbBK1DyAInPleGrQw71X

23/01/2026

Mkuu wa majeshi nchini Uganda ambaye pia ni mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugana amesema siku ya Ijumaa kuwa wanachama 30 wa upinzani wameuawa na watu 2,000 kuk**atwa baada ya uchaguzi.

“Tumewak**ata zaidi ya wahuni 2,000 ambao Kabobi alidhani angewatumia,” aliandika mkuu wa majeshi Jenerali Muhoozi Kainerugaba kwenye mtandao wa X, akitumia jina la kumkejeli Bobi Wine (Kabobi).

“Mpaka sasa tumewaua magaidi 30 wa NUP,” alisema, akiashiria chama cha Bobi Wine, cha National Unity Platform (NUP).

Kiongozi wa upinzani Bobi Wine bado yuko mafichoni baada ya kushtumu vikosi vya usalama kwa kuvamia nyumba yake kufuatia uchaguzi uliofanyika Januari 15.

Fuatilia kituo cha KILINGENI kwenye WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VbBK1DyAInPleGrQw71X

20/01/2026

Chama cha upinzani cha People's Front for Freedom nchini Uganda kinachoongozwa na Kizza Besigye, kimesema leo kuwa afya ya kiongozi huyo aliyefungwa inadhoofika, baada ya kukimbizwa usiku kwenye kituo cha matibabu katika mji mkuu wa Kampala.

Katika taarifa yake, chama hicho kimesema kuwa Besigye yuko katika hali mbaya kiafya. Aidha, kimetoa wito kwa maafisa wa Uganda kuhakikisha madaktari binafsi pamoja na familia yake wanaonana naye bila vikwazo vyovyote.

Chama hicho kimeendelea kusema ni jambo la kusikitisha kwamba mtu ambaye amejitolea maisha yake kwa afya na uhuru wa wengine ananyimwa haki yake ya kupata utu wa matibabu.

Kwa upande wake, msemaji wa mfumo wa magereza nchini humo Frank Baine, amekanusha taarifa hiyo .

Fuatilia kituo cha KILINGENI kwenye WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VbBK1DyAInPleGrQw71X

20/01/2026

Ananionaje?

20/01/2026

Simba SC imetambulisha ingizo jipya la tatu kwa maana wachezaji wapya kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Asubuhi ya leo Wekundu wa Msimbazi wameweka hadharani kuingia mkataba wa miaka miwili na beki wa kati, Ismael Olivier Traore kutoka Falme za Kiarabu.

Mwamba huyo ana uzoefu na soka la Afrika baada ya kucheza Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa akiwa na timu k**a vile Asec Mimosas, Marumo Galants na Stellenbosch.

Usajili huo wa raia huyo wa Ivory Coast unakuwa ni wa tatu mpaka sasa baada ya awali kutambulishwa winga, Lebasse Guey na mbavu ya kushoto, Nickson Kibabage.

Wakati huo taarifa za ndani zikieleza muda wowote atatambulishwa kiungo wa mpira, Clatou Chota Chama ambapo atakuwa anarejea nyumbani kwa mara ya tatu.

Fuatilia kituo cha KILINGENI kwenye WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VbBK1DyAInPleGrQw71X

Photos from MTEULETHEBEST.COM's post 19/01/2026

Kifurushi cha kurudi cha chombo cha anga cha Shenzhou-20, kisicho na wanaanga, kilitua katika eneo la kutua la Dongfeng kaskazini mwa Ukanda wa Kujiendesha wa Mongolia ya Ndani ya China saa 3:34 asubuhi (Saa za Beijing) Jumatatu xhtxs.cn/9DB

Fuatilia kituo cha KILINGENI kwenye WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VbBK1DyAInPleGrQw71X

Telephone