Imara Tech

Imara Tech

Share

Ofisini kwetu ipo SIDO grounds, Arusha, Tanzania.

Imara Tech is a Tanzania-based social enterprise start-up that manufactures agricultural equipment for smallholder farms.

~~~~~~~~
Imara Tech ni kampuni mpya ya kutengeneza teknolojia ya mbalimbali.

09/09/2026

CHAFF CUTTER-MASHINE MOJA, MATUMIZI MENGI

Unatafuta mashine imara ya kukata na kusaga malisho pamoja na mazao mbalimbali? Chaff Cutter yetu inapatikana kwa options tofauti kulingana na mahitaji yako.

Chaff Cutter ya Umeme – Single Phase | TSh 1,900,000
Chaff Cutter ya Petrol – HP 8 | TSh 1,700,000
Mega Chaff Cutter ya Diesel – HP 25 | TSh 5,500,000

Mashine hizi zinafaa kwa:
• Kukata majani mabichi na makavu
• Kubaraza mahindi
• Kusaga magunzi
• Kusaga mabua
• Kusaga mashudu
• Kusaga dagaa

Chagua mashine kulingana na mahitaji na uzalishaji wa biashara yako.

Kwa maelezo zaidi na kuagiza, tupigie/WhatsApp: 0678 343 826

Imara Tech-Kamata Fursa, Badili Maisha.

Photos from Imara Tech's post 07/09/2026

Kutoka shambani hadi kwenye uzalishaji, Imara Tech tunakuletea mashine zinazobadilisha namna wakulima na wafugaji wanavyofanya kazi. Punguza muda na nguvu zinazotumika kwenye shughuli za kilimo na ongeza ufanisi kwa kutumia mashine bora za Imara Tech.

Imara Tech-Kamata Fursa, Badili Maisha

03/09/2026

Wiki moja hadi Siku moja! 🔥

Hivi ndivyo wateja wetu kutoka Goma, DRC Congo 🇨🇩 wanavyoshuhudia nguvu ya mashine za Imara Tech kwenye upigaji wa maharage.

Kabla ya kutumia mashine zetu, kazi ilikuwa inachukua hadi wiki 1. Leo? Siku 1 tu! 🙌🏽

Teknolojia sahihi = muda mchache, kazi rahisi na uzalishaji mkubwa.

Imara Tech-Kamara fursa,badili maisha.

Photos from Imara Tech's post 02/09/2026

Hongera kwa Mkurugenzi wetu, Alfred Chengula kwa kutunukiwa tuzo ya PABRA Youth and Women Entrepreneurship Award! 🏆

Tuzo hii ni utambuzi wa uongozi bora na mchango wake katika kukuza biashara zinazoongozwa na vijana na wanawake, hususan katika mnyororo wa thamani wa maharage, uzalishaji wa mbegu, uchakataji, masoko na maendeleo ya kilimo-biashara.

Tunajivunia uongozi wako, maono yako na juhudi zako za kuleta suluhisho za kiteknolojia kwa wakulima na wafanyabiashara.

Hongera sana Mkurugenzi! Tuzo hii ni ushahidi kwamba kazi yetu inaacha alama.

Photos from Imara Tech's post 01/09/2026

Wateja wetu kutoka Goma, DRC Congo wakifurahia matokeo baada ya kutumia mashine zetu katika kupigia maharage.

“Zamani tulikuwa tunatumia wiki moja kumaliza kazi, lakini baada ya kutumia mashine za Imara Tech, sasa tunamaliza ndani ya siku moja!” wamezungumza wakulima hao.

Hii ndiyo nguvu ya teknolojia kwenye kilimo,kuokoa muda, kupunguza nguvu kazi na kuongeza ufanisi.

Imara Tech, tunakuletea mashine zinazobadilisha namna unavyofanya kazi.Wewe bado unatumia nguvu nyingi? Ni wakati wa kubadilika.

Imara Tech-Kamata fursa, badili maisha.

Photos from Imara Tech's post 31/08/2026

ASANTENI MARA!

Tunaishukuru sana jamii ya Mara kwa mapokezi mazuri na upendo mliotuonyesha wakati wa Maonesho ya Madini yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyamongo, North Mara Gold Mining.

Kuanzia tarehe 25 hadi 29 Agosti 2026, tumefurahi kukutana nanyi, kuzungumza nanyi na kuwafikishia fursa mbalimbali kutoka Imara Tech.

Mara, mmeonyesha upendo wa kipekee. Asanteni kwa kutupokea, kutuamini na kutupa nafasi ya kuwa sehemu yenu.

Imara tech-Kamata fursa badili maisha.

29/08/2026
27/08/2026

Tunapita mtaa kwa mtaa kuhakikisha tinakupatia elimu na tunakueletea fursa hadi mlangoni kwako🔥🔥🔥 Hii ndo Imara tech ushindwe wewe tu kukamata fursa🔥

Imara tech-kamata fursa,badili maisha

Photos from Imara Tech's post 26/08/2026

Ground Activation yetu mtaa kwa mtaa inaendelea! 🚜🌾 Tupo North Mara kwenye maonesho yanayoendelea hadi Agosti 29, 2026, tukiwaletea wakulima na wafugaji teknolojia bora za kilimo moja kwa moja karibu nao.

📍 Nyamongo, North Mara

Tunafika hadi mtaani kwako!
Tuambie ulipo, tukuletee fursa karibu na wewe.

Karibu uone mashine zetu, ujifunze namna zinavyofanya kazi na uchague teknolojia itakayokusaidia kuongeza uzalishaji na kipato.

Imara Tech – kamata fursa, badili maisha!

Photos from Imara Tech's post 26/08/2026

NYAMONGO, TUMEFIKA,

Maonesho ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Nyamongo, North Mara, yameanza tarehe 25 na yatafikia tamati tarehe 29 Agosti 2026.

Na sisi Imara Tech tupo hapa,
Karibu kwenye banda letu ujionee mashine zetu, pata maelezo zaidi na ujue namna teknolojia inaweza kukusaidia kuongeza uzalishaji na kukuza biashara yako.

📍 Viwanja vya Nyamongo – North Mara
📅 25–29 Agosti 2026

Usipite Nyamongo bila kututembelea!
Imara tech-kamara fursa, badili maisha

Want your business to be the top-listed Engineering Company in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


SIDO Plot 42, Unga Limited
Arusha

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:30
Tuesday 09:00 - 17:30
Wednesday 09:00 - 17:30
Thursday 09:00 - 17:30
Friday 09:00 - 17:30
Saturday 09:00 - 17:30