Mr Meshacking

Mr Meshacking

Share

MUNGU NI MWEMA
(GOD IS GOOD)

20/09/2026

Kijana alikuwa anaitwa Issa yeye aliishi maisha ya kawaida katika kijiji kilichokuwa karibu na msitu. Kazi yake kubwa ilikuwa kukata mkaa ili kujipatia kipato cha kuendesha maisha yake.

Kazi hiyo haikuwa rahisi. Kila alipokwenda msituni, alilazimika kuwa makini sana kwa sababu mara kwa mara alikutana na askari wa wanyamapori waliokuwa wakifanya doria. Wakati mwingine walimkimbiza, na wakati mwingine walizozana naye kwa sababu walimkuta akikata miti kwa ajili ya mkaa.

Pamoja na changamoto hizo, kijana huyo aliendelea na kazi yake kwa sababu alikuwa na kibali cha kufanya shughuli hiyo katika eneo aliloruhusiwa.

Siku moja, k**a kawaida yake, aliamka mapema na kuelekea msituni. Alikuwa na vifaa vyake vya kazi na alikuwa amedhamiria kukamilisha kazi yake kabla ya kurudi nyumbani.

Akiwa njiani, alipita katika sehemu iliyokuwa na vichaka vingi na miti midogo. Ghafla, macho yake yakagundua kitu kilichokuwa kimelala chini.

Aliposogea karibu, akashangaa kuona bunduki ikiwa imedondoka chini.

Kijana huyo akasimama na kuitazama kwa muda. Akaangalia huku na huku kuhakikisha hakuna mtu aliyekuwa karibu.

Baada ya kusita kidogo, akaichukua ile bunduki. Kwa kuwa alikuwa amebeba gunia la mkaa, akaificha ndani ya mzigo wake wa mkaa na kuendelea na safari.

Baadaye alipomaliza kazi, alirudi nyumbani akiwa na mzigo wake. Bunduki hiyo aliificha ndani ya nyumba yake, akiamini kwamba hakuna mtu aliyejua kuwa alikuwa ameipata.

Alikaa kimya akisubiri muda wa kupika ufike.

Lakini wakati huo, aliamua kuwasha televisheni ili kupata habari za siku hiyo.

Alikuwa bado hajui kwamba habari aliyokuwa karibu kuisikia ingebadilisha kabisa mawazo yake.

Mtangazaji wa habari akatangaza:

“Bunduki ya askari wa wanyamapori imeibiwa na mtu asiyejulikana.”

Kijana yule akashtuka.

Akatazama televisheni kwa makini.

Habari ikaendelea kueleza kuhusu bunduki hiyo na tukio lilivyotokea. Walionyesha pia picha ya bunduki iliyokuwa ikitafutwa.

Moyo wake ukaanza kwenda mbio.

Akaondoka pale alipokuwa

18/09/2026

Sikiliza kwa makini mpaka mwisho, kisha tuambie umejifunza nini..

18/09/2026

**a ya Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma imemhukumu Rajabu Uhuru (36), Dereva wa bodaboda na Mkazi wa Kijiji cha Ilalangulu, kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka Mtoto wa k**e mwenye umri wa miaka 13.

Akisoma hukumu hiyo Septemba 17, 2026, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahak**a hiyo, Misana Majula amesema Mahak**a imejiridhisha pasipo shaka kupitia ushahidi uliowasilishwa na Upande wa Mashtaka kuwa Mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Mahak**a imeeleza kuwa kosa hilo lilitendwa Juni 12, 2026, majira ya saa 3 usiku katika eneo la Kigulwe, Kijiji cha Ilalangulu, Kata ya Mtego wa Noti, Tarafa ya Nguruka, wilayani Uvinza.

Baada ya tukio hilo, Uhuru alitoroka na kwenda kujificha Jijini Dar es salaam kwa lengo la kukwepa mkono wa sheria, lakini kupitia upelelezi wa Jeshi la Polisi alibainika alikokuwa amejificha na kuk**atwa.

Hukumu hiyo imeelezwa kuwa sehemu ya utekelezaji wa sheria katika kulinda haki za watoto na kukabiliana na vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia .

15/09/2026

Kwa Mavondo Tz – Nimetambuliwa sasa hivi k**a mmoja wa mashabiki wake bora!

25/08/2026

fans Unaye muona pichani hapo ni Mbabe wa kivita wa Liberia, anaitwa Prince Yormie Johnson, Huyu ndie aliye ongoza operation ya kuk**atwa raisi wa Liberia Samuel Kanyon Doe kisha akateswa, na kuuawa Septemba 1990.

Johnson alikuwa akiongoza Kundi la waasi wa "Independent National for Patriotic Front of Liberia" (INPFL), Vikosi vyake ndio vilio mk**ata raisi Doe baada ya kumvizia pale Freeport Monrovia.

Baada ya kuk**atwa, Samuel Doe alipelekwa kwenye kambi ya INPFL ambapo huko Johnson alisimamia mahojiano na kisha mateso dhidi ya Doe.

Rais Doe alikatwa masikio huku akirekodiwa kwenye video, kisha akaburuzwa mitaani na kupigwa kipigo kikali akiwa uchi.

Doe alifariki kutokana na majeraha na mateso aliyopata kutokana na mateso kutoka kwa askari wa Johnson.

17/08/2026

Mwaka 2015, ISIS ilikata vichwa vya wanaume 20 Wakristo ambao walikataa kumkana Kristo.

Kulikuwa pia na mtu mmoja aliyeitwa Matthew Ayariga, mfanyakazi kutoka Ghana aliyekuwa amehamia Libya kutafuta kazi. Wakati huo, hakuwa Mkristo, lakini alijikuta akiwa pamoja na wale waliotekwa na ISIS. ISIS ilimwambia kwamba angeweza kuachiliwa na kupewa uhuru ikiwa tu angemkana Kristo.

Lakini baada ya kuwaona wale wanaume wa imani wakisimama imara na kukataa kumkana Kristo, kwa ujasiri alisema:

“Mungu wao ni Mungu wangu.”

Ayariga aliamua kufa pamoja na wale Wakristo badala ya kuikana imani yao.
Reposted from David Mmbaga

10/08/2026

【Agosti 9】 Siku ya Maombi ya Amani ya Kuwakumbuka Waathirika wa Bomu la automic (Nyuklia) la Nagasaki

Picha hii inamuonyesha mvulana mdogo, ambaye licha ya umri wake, amembeba mgongoni mdogo wake aliyefariki kwa ujasiri na uthabiti mkubwa, huku akisubiri zamu yake ya kuchomwa moto.

Picha hiyo ilipigwa na Joe O'Donnell, sajenti wa Jeshi la Wanamaji la Marekani na mpiga picha wa kijeshi.

Wakati huo alikuwa kijana mwenye umri wa miaka 23. Baadaye aliandika katika kumbukumbu zake:

"Nilitaka kumkumbatia yule mvulana, lakini nilihisi kwamba nikifanya hivyo, huenda nikavunja moyo na roho yake iliyokuwa ikijizuia kwa nguvu kubwa, hivyo sikuweza."

Nilikuwa nimeingia Nagasaki nikitokea Sasebo, na nilikuwa nikitazama chini kutoka juu ya kilima kidogo. Ndipo nilipowaona wanaume waliovaa barakoa nyeupe. Walikuwa wakifanya kazi karibu na shimo walilokuwa wamelichimba, lenye kina cha takribani sentimita 60. Walikuwa wakiweka miili iliyokuwa imepangwa juu ya mkokoteni, mmoja baada ya mwingine, ndani ya shimo lililotumika kuchomea kwa chokaa.

Macho yangu yalivutiwa na mvulana wa takribani miaka 10 aliyekuwa akipita. Alikuwa amefunga kamba ya kumbebea mtoto begani na alikuwa amembeba mtoto mdogo mgongoni. Japokuwa wakati huo nchini Japan ilikuwa jambo la kawaida kuwaona watoto wakicheza katika maeneo ya wazi huku wakiwa wamewabeba wadogo zao mgongoni.

Lakini kulikuwa na tofauti kubwa katika mwenendo wa mvulana huyu. Niliweza kuhisi ndani yake dhamira kubwa, kana kwamba alikuwa amekuja katika eneo hili la kuchomea miili akiwa na kusudi zito sana. Zaidi ya hayo, alikuwa hana viatu.

Mvulana huyo alipofika ukingoni mwa eneo la kuchomea miili, alisimama bila kusogea, akitazama kwa makini huku uso wake ukiwa mgumu na wenye huzuni. Mtoto aliyekuwa mgongoni mwake alikuwa amelala usingizi mzito au mwili wake ulikuwa umedhoofika kabisa, huku kichwa chake kikiwa kimeanguka nyuma.

Inaonekana mvulana huyo alisimama pale ukingoni kwa dakika tano au kumi. Wanaume waliovaa barakoa nyeupe walimkaribia taratibu na kuanza kufungua kamba aliyokuwa ameitumia kumbeba mtoto.

Hapo ndipo nilipotambua kwa mara ya kwanza kwamba mtoto aliyekuwa mgongoni mwake alikuwa tayari amefariki.

Wale wanaume walimshika mtoto huyo mikono na miguu, kisha wakamlaza kwa upole juu ya majivu yaliyokuwa moto katika eneo la kuchomea miili, kana kwamba walikuwa wakifanya ibada ya mazishi.

Kwanza kulisikika sauti ya nyama changa ikiyeyuka kwa joto la moto. Kisha, ghafla, mwali mkali wa moto uliruka juu.

Mwali huo, k**a machweo mekundu yenye kuvutia, uliangaza mashavu yaliyokuwa bado ya kitoto ya yule mvulana aliyekuwa amesimama wima bila kutikisika.

Ndipo nilipoona damu ikitoka kwenye midomo ya mvulana huyo, ambaye alikuwa akitazama moto bila kupepesa macho. Kwa sababu alikuwa amekaza meno yake kwa nguvu sana, damu kutoka kwenye mdomo wake haikutiririka, bali ilibaki ikipaka sehemu ya chini ya mdomo wake rangi nyekundu.

Miale iliyokuwa k**a machweo ilipopungua, mvulana huyo aligeuka ghafla na kuondoka kimya kimya kutoka eneo lile la kuchomea miili.

Huko Nagasaki na Hiroshima, simulizi k**a hizi, pamoja na picha na kumbukumbu za mashahidi, zimekuwa zikihifadhiwa na kupitishwa kwa vizazi vijavyo.

Lakini bila shaka, makumi ya maelfu ya watu wengine walioteketezwa papo hapo walikuwa na hadithi zao wenyewe. Walikuwa na maisha waliyotamani kuyaishi kwa ukamilifu zaidi, ndoto walizokuwa nazo, na maisha ya baadaye yaliyokuwa mbele yao.

Miaka 81 baada ya vita, inasemekana kwamba idadi ya watu ambao waliupitia moja kwa moja wakati huo imepungua hadi takribani asilimia 10.

Na kadiri miaka inavyopita, tunaona wanasiasa na vijana zaidi duniani wakisema kwa urahisi kauli k**a, “Bomu la atomiki lilikuwa na gharama nafuu.”

Lakini jambo ambalo hatupaswi kamwe kulisahau ni kwamba, kwa namna fulani, ni bahati tu kwamba sisi ndio tuko hai leo.

Lakini ingekuwa ni wazazi wetu au babu na bibi zetu waliokuwa pale?

Tunapolitazama jambo hili kwa mtazamo huo, tunatambua kwamba hakuna sababu yoyote ya kuhalalisha vita.

Nyuma ya kila namba ya waliokufa kuna mtu aliyekuwa na jina, familia, ndoto, matumaini na maisha ambayo alitamani kuyaishi.

Tusiache historia ipotee. Tukumbuke yaliyopita ili vizazi vijavyo vijifunze kuchagua amani badala ya vita. 🕊️

Photos from Mr Meshacking's post 10/08/2026

MAMBO 10 NILIYOYAONA SIMBA SC vs POLICE FC KENYA

1️⃣ Kwanza kabisa, hii ilikuwa bonanza. Pengine kwenye mechi za aina hii kiwango cha ufundi na umakini wa makocha huwa si kikubwa sana. Unaweza kuona wachezaji wakicheza nje ya nafasi zao na mfumo wa uchezaji kutokuwa na organization kubwa.

2️⃣ Simba ina utajiri mkubwa sana wa mawinga. Lakini swali langu ni hili: kwa nini timu haijaenda sokoni kutafuta namba 10 mwenye level ya Chama? Ukiwa na mawinga wengi, unahitaji mtu wa kati anayejua kuwapa mipira na kuunganisha mchezo.

3️⃣ Kipindi cha kwanza Simba ilikuwa inaflow vizuri, lakini tatizo kubwa lilikuwa kwenye ubunifu wa kutengeneza nafasi. Mipira ilikuwa inafika mbele, lakini kulikuwa na ukosefu wa mtu wa mwisho anayejua kuifungua defense ya mpinzani. Namba 10 hakuwa kwenye kiwango nilichotarajia.

4️⃣ Kipindi cha pili flow ilipungua, lakini baada ya kuingia Chama ukaona tofauti. Simba ikaanza kufika kwenye eneo la mpinzani kwa ubunifu zaidi. Chama alileta kitu ambacho Simba ilikuwa inakikosa—ubunifu na decision making kwenye eneo la mwisho.

5️⃣ Steve Barker ana kazi moja kubwa: achague moja. Ama Simba iende sokoni kutafuta namba 10 wa kiwango cha juu, au Maema na Morice Abraham wanahitaji kuzaliwa upya . Vinginevyo Chama atacheza mpaka akiwa na miaka 50 kwa sababu bado utaona umuhimu wake kwenye mfumo huu.

6️⃣ Loemba nimempenda zaidi akiwa defensive midfielder. Leo nimeona intensity yake, uwezo wa kukimbia, kushindana na kushiriki kwenye ulinzi. Kwangu mimi, akiwa nyuma kidogo anakuwa na impact kubwa zaidi kuliko kumlazimisha kuwa attacking midfielder.

7️⃣ Ibrahim Jabaar ni mtu wa kutuliza kiungo. Anapokea mpira vizuri, anajua kupeleka mchezo mbele na pasi zake zina maana. Huyu ni aina ya midfielder anayesaidia timu isitawanyike inapokuwa na presha.

8️⃣ Eneo la mbele la Simba bado linahitaji ubunifu zaidi na striker mwenye uwezo wa hali ya juu. Timu inapokutana na mpinzani anayekaa nyuma, mambo yanakuwa magumu sana k**a

09/08/2026

Dr Besige alikuwa ni Daktari wa Museveni kwa karibu miaka 10 mstuni, aliokoa maisha yake wakati wote huo, Sasa ebu angalia Museveni anavomtesa Dr Kiza Besigye kwa sasa.

Ama kweli.... Tenda Wema Bila Kutarajia Malipo, Sababu Wahenga Wanasema Kamwe Mto Hauwezi Kunywa Maji Yake, Na Mti Hauwezi Kula Matunda Yake.

Follow me on facebook fans

30/07/2026

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Rahma Musa Tito (16), mkazi wa Kijiji cha Msoga, Wilaya ya Chalinze, kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi, Hadija Hemedi Shaha (51), ambaye alikuwa mkulima na mwenye ulemavu wa miguu yote miwili.

Kwa mujibu wa Polisi, tukio hilo lilitokea usiku wa Julai 28, 2026, majira ya saa 5:00, baada ya marehemu kumzuia binti yake kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya rafiki yake iliyokuwa ikifanyika karibu na Hospitali ya Msoga, iInadaiwa kuwa Mtuhumiwa alianza kumshambulia mama yake kabla ya kumchoma kichwani kwa kutumia kitu chenye ncha kali.

Aidha, asubuhi ya Julai 29, 2026, Fundi ujenzi aliyekuwa akidai malipo na kufuata mfuko wa saruji alifika Nyumbani kwa marehemu, baada ya kugonga mlango, alifunguliwa na Rahma Musa Tito, ndipo alipobaini mwili wa Hadija Hemedi Shaha ukiwa umelala sakafuni na ukiwa na majeraha kichwani yaliyokuwa yakivuja damu.

Jeshi la Polisi limesema Mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano na hatua nyingine za kisheria zinaendelea huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea ili kubaini mazingira yote yaliyosababisha mauaji hayo.

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Arusha