Ps. Emmanuel Cliff

Ps. Emmanuel Cliff

Share

Turning People to Become God's Sons. Galatians 4:7

07/10/2026

✍ Mtu Asipotee
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa apotee.
Mathayo 18:14 SRUV
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Ulishawahi kufanya kosa na ukadhani kwamba Mungu amekuacha? Habari njema ni hii, haiwezekani Mungu kumuacha mtu hata k**a ni mbaya na muovu. Mungu hataki upotee!

Mathayo 18:12-13
12 Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je! Hawaachi wale tisa na tisini, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea?

13 Hata akipata kumwona, amin, nawaambia, amfurahia huyo zaidi, kuliko wale tisa na tisini wasiopotea.

Mungu anao watu wengi sana ambao wanamuamini, wanampenda na wanamtii Yeye; lakini, ikitokea mmoja wao akapotea na kutoka kwenye kundi, Mungu hamuachi, atamtafuta mpaka ampate.

Mwanadamu ni wa thamani kuliko vitu vyote ambavyo Mungu anavimiliki, hawezi kukubali kumpoteza mwanadamu kwa namna yoyote ile. Mtu mmoja akipotea, Mungu atamtafuta mpaka ampate.

K**a kuna mtu ambaye alikuwa akimuamini Mungu lakini ikatokea akamuacha, na unamfahamu, basi fanya kazi ya Mungu ya kuhakikisha unamfuata ili kumrejesha. Ndivyo Mungu anavyotaka!

K**a unadhani umemkosea Mungu sana kiasi kwamba amekuacha, basi nikwambie tu, kwa namna ambavyo Mungu anakupenda, haiwezekani kukuacha hata k**a kuna kosa umetenda.

Makosa yako sio kitu mbele ya upendo wa Mungu.

Usimkimbie Mungu, mkimbilie. Neema yake ni kubwa kuliko makosa yako; kuwa na amani, Mungu hajakuacha na hawezi kukupungukia kwa chochote. Mungu ni wako na wewe ni wa kwake milele yote.

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Baba Yangu na Mungu Wangu Nakutukuza Kwa Kuwa Neema Yako Inafanya Kazi Maishani Mwangu, Neema Yako ni Kuu Kuliko Makosa Yangu. Asante Kwa Upendo Wako Mzuri, Nina Amani Kwa Kuwa Wewe ni Upendo. Amen

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Yakobo 5:19-20
19 Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza;

20 jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi.

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).

Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

06/10/2026

✍ K**a Mtoto Mdogo
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Marko 10:15 SRUV
Amin, nawaambieni, yeyote asiyeukubali ufalme wa Mungu k**a mtoto mdogo hatauingia kabisa.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Neno linatutaka kuwa k**a watoto wadogo linapokuja swala la Ufalme wa Mungu. Kwa sababu kanuni za ufalme wa Mungu haziingii akilini.

Ufalme wa Mungu ni wa kuukubali k**a ambavyo upo bila kujiuza, ndio maana tunafundishwa kuhusu imani. Ufalme wa Mungu unakutaka kuamini tu pasipo kujua itakuwaje. Mungu tayari anajua!

Kanuni za Mungu za mafanikio yako sio k**a za ulimwengu; hapa duniani imani ipo kwenye elimu na kufanya kazi kwa bidii zote. Na ndio maana wanafanikiwa kwa taabu ikiambatana na magonjwa.

Ufalme wa Mungu unataka ufanye kazi lakini usitegemee kazi wala usitegemee nguvu zako kabisa; umtegemee Mungu na kufuata kanuni za Mungu za baraka na mafanikio.

Ufalme wa Mungu unaongozwa na Neno la Mungu ambalo unapaswa kulitenda pasipo kujiuliza maswali, unakubali tu na kufanya ukiamini kwamba Mungu atatenda k**a alivyosema kwenye neno lake.

Mungu ana neno kwa ajili ya kila kitu kuhusu wewe, k**a unataka kufanikiwa ni lazima ufuate neno hilo la Ufalme (kanuni), na kwa kufuata kanuni hizo utapata kila kitu na kufanikiwa katika kila kitu.

Mungu anataka umuamini Yeye, ujue kwamba alichokisema ni kwa mafanikio yako. Huwezi kuona kile ambacho Mungu amepanga lakini ukifanya sawasawa na neno lake utaona matokeo mazuri.

Kuwa k**a mtoto, pokea neno la Mungu na ufanye k**a neno linavyotaka ufanye. Mungu anakupenda sana na utaona matunda ya kutii neno la Mungu, utaishi maisha mazuri na ya mafanikio.

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Baba Yangu na Mungu Wangu Mzuri, Asante Kwa Kuwa Neno Lako ni Muongozo Wa Maisha Yangu. Baba Asante Kwa Kuwa Kila Ninapolifanya Neno Lako, Linanipa Matokeo Sawasawa na Neno Linavyosema. Amen

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao, akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa k**a watoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Mathayo 18:2-3 SRUV

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).

Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

06/10/2026

✍ Hakuna Lisilowezekana
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Mattayo MT. 17:20 SWZZB1921
Yesu akawaambia, Kwa sababu ya kutokuamini kwenu. Kwa maana, amin, nawaambieni, Mkiwa na imani k**a punje ya kharadali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa hata kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Wanafunzi wa Bwana Yesu walishindwa kutoa pepo la kifafa, na hawakujua ni kwa sababu gani walishindwa. Kwa kuwa ni watu waliopenda kujifunza, hawakutulia, walitaka kujua sababu zilizowafanya washindwe.

Ukisoma Mathayo 10 utaona wanafunzi wa Bwana Yesu wakitumwa kwenda kuhubiri habari njema za Ufalme wa Mungu na kuponywa, kufufua nk. Walishangaa kwa nini washindwe kutoa pepo tena.

Bwana Yesu anawaambia tatizo ni "kutokuamini," kwa maana wangekuwa na imani, wangeliambia pepo litoke na lingetoka; isingeshindikana kutoka kwa sababu ya imani. Imani inaweza mambo yote!

Mungu anaweza mambo yote, akakuumba wewe pia ili mambo yote yawezekane kwako; na ili kufanikisha hilo, akakupa imani ile ile ambayo Bwana Yesu alikuwa anayo na akaitumia kutenda mambo makuu.

Imani tayari unayo, je! Utachangua kuamini au kutokuamini? Kuna mtu anaomba lakini haamini k**a atapewa, huyo hawezi kupewa. Imani inakupa sawasawa na unavyoamini.

Imani ni kuwa na uhakika kwamba kipe unachotamka kitakuwa k**a ambavyo umetamka. Kile ulichoomba utakipata k**a ambavyo umekiomba na sio vinginevyo. Ukiamini hakuna kinachoshindikana.

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Nina Imani Ya Kuhamisha Milima, Chochote Ninachotamka Nina Uhakika Kwamba Kitatokea K**a Nilivyotamka. Sina Mashaka, Sina Wasiwasi na Siyumbi Juu ya Kile Nilichotamka.

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Marko 11:23 SRUV
Amin, nawaambia, yeyote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).

Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

05/10/2026

✍ Ukiongea Litatendeka
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Mathayo 21:21
Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng'oka, ukatupwe baharini, litatendeka.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Je! Unajua kwamba kila kitu hapa duniani kimeumbwa kwa neno? Na kwa kuwa kimeumbwa kwa neno, kinatii kila neno. Hata maneno mabaya yanafanyika k**a yametamkwa.

Neno letu la leo kwa kifupi linatupa ujumbe kwamba "tukitamka kitu kitatendeka." Ndio, k**a hutamki kitu kwa sababu una imani kuwa Mungu anajua hitaji lako tayari, basi hutaona chochote kikitokea.

Mwanadamu ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, amepewa uwezo wa kuongea maneno yanayoeleweka na yaliyobeba mamlaka. Hakuna kitu chochote kinaweza kuzuia neno lako.

Mungu hazuii neno baya ulilotamka kwamba lisitokee, hapana, ataacha na litatokea k**a ulivyotamka kwa sababu amekupa uwezo wa kuumba na kutii vitu vyote kwa mdomo wako.

Kila kitu kinakusikiliza wewe, ufalme wa Mungu pia unakusikiliza wewe; chochote unachotamka hakuna kiumbe kinaweza kubishana na wewe hapa duniani. Unayo amri kwenye kinywa chako.

Unachotamka kuhusu afya yako ndivyo itakavyokuwa. Unavyotamka kuhusu kazi zako ndivyo itakavyokuwa; ukisema chochote na ukaamini kuwa kitatokea, hicho kitu ulichotamka kitatokea.

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Baba Mpendwa Asante Kwa Kunipa Neno Lako Kinywani Mwangu, Neno Lako Lina Nguvu za Kuumba Kila Kitu. Naamini Ninapolitamka Linatendeka K**a Ambavyo Nimelitamka. Hallelujah!

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Mathayo 17:20 SRUV
Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).

Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

05/10/2026

✍ Ndoto na Sadaka
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Mwanzo 28:22
Na jiwe hili nililolisimamisha k**a nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Ndoto ni njia nyingine ambayo Mungu anaitumia kuzungumza na sisi watoto wake, tatizo ni kwamba watu wanadhani ndoto ni ndoto tu ila ndoto zina maana na zinaweza kukusaidia.

Mungu alizungumza na Abraham na kufanya nae maagano na ahadi kwa njia ya ndoto, na zikatimia kwamba sababu aliamini kwamba ni Mungu anazungumza nae.

Yakobo aliota ndoto akiona ngazi zimepanda kutoka alipo mpaka mbinguni, malaika wakishuka na kupanda. Katika hiyo ndoto Mungu akazungumza nae, neno linatuambia;

Mwanzo 28:13-15
13 Na tazama, Bwana amesimama juu yake, akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako.

14 Na uzao wako utakuwa k**a mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa.

15 Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.

Baada ya ndoto hii iliyojaa ahadi kutoka kwa Mungu, Yakobo aliahidi kumpatia Mungu matoleo ya sehemu ya kumi ikiwa kiwa Mungu atamtendea k**a alivyo-ahidi kwa njia ya ndoto.

Yakobo hakuwa na kitu cha kutoa wakati huu, ila, Abraham kila wakati Mungu alipozungumza nae katika ndoto alimtolea Mungu sadaka ya kupokea kile kile au ahadi ambayo Mungu alimwambia.

Ndoto yoyote nzuri ambayo Mungu amekupatia, itolee sadaka. Kwa kufanya hivyo unakuwa umeipokea, imekuwa yako na itatokea k**a vile ulivyoona kwenye ndoto. Usidharau ndoto!

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Baba yangu na Mungu wangu, nimejifunza kuhusu ndoto na sasa ninajua nini cha kufanya; zungumza na mimi na nionyeshe mapenzi yako kwangu nami nitayapokea kwa imani na shukrani. Amen

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Mwanzo 12:7
Bwana akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu Bwana aliyemtokea.

Mwanzo 28:16, 20-22
16 Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua.

20 Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;

21 nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu.

22 Na jiwe hili nililolisimamisha k**a nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).

Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

04/10/2026

✍ Nuru Yenu Iangaze
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Mathayo 5:16 NEN
Vivyo hivyo, nuru yenu iangaze mbele ya watu, ili wapate kuona matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Unajua kwamba wewe ni nuru ya huu ulimwengu wenye giza? Unajua kwamba popote ambapo wewe utatokea lazima utaangaza? Huwezi kujificha kwa sababu wewe ni nuru ya huu ulimwengu.

Shetani anajua kwamba wewe ni nuru, anaiona nuru yako lakini anajitahidi kwa nguvu zote kujaribu kukuonyesha kwamba huna ambacho unaweza kufanya mahali ambapo amefanya uharibifu.

Shetani ni giza na kazi zake zote ni giza, Mungu alivyo mzuri akakufanya wewe uwe nuru kwa njia ya Yesu Kristo ili unapotokea mahali palipo na giza, giza lote likimbie, sio wewe ukimbie.

Hakuna giza linaloweza kujificha mahali ambapo kuna nuru, hakuna mapepo yanaweza kufanya kazi na kufanikiwa mahali ambapo wewe upo. Umebeba nuru ya Kristo na umefanywa kuwa nuru.

Neno linasema "nuru yenu iangaze mbele ya watu, ili wapate kuona matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni." Ili watu wajue kuwa wewe ni nuru, wanaangalia matendo yako.

Unapokutana na wagonjwa unafanya nini, Utawaponya au utawaacha? Je ukikutana n walio na hali mbaya kimaisha na una uwezo wa kuwasaidia, utawasaidia? Nuru yako inaonekana kwa matendo.

Unavyoishi na watu ndivyo ambavyo wanazidi kutambua kwamba wewe ni nuru na wanaelewa kwamba unae Mungu. Hakikisha matendo yako yanamtangaza Mungu hapa duniani.

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Mimi ni Nuru ya Ulimwengu, Popote Ninapokua Watu Wanamuona Kristo, Wanaona Huruma Zake na Upendo Wake Katika Kuponya, Kuwaokoa na Kuwapatia Mahitaji Yao. Hallelujah!

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Mathayo 5:14-15 NEN
Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojengwa kilimani hauwezi kufichika. Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa bakuli. Badala yake, huiweka kwenye kinara chake, nayo hutoa mwanga kwa kila mtu aliye ndani ya ile nyumba.

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).

Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

04/10/2026

✍ Habari Njema
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Mathayo 9:35 NEN
Yesu akazunguka katika miji yote na vijiji vyote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri habari njema za ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Ukisikia Bwana Yesu alifundisha habari njema, ni habari njema kweli zinazohusu Ufalme wa Mungu. Alikuja na habari njema ya kututoa kwenye dhambi ambazo zilileta laana za kila namna.

Laana ameiondoka kwako kwa kuleta baraka maishani mwako. Umebarikiwa, wewe umefanyika kuwa baraka, wewe sasa ni baraka kwa watu wote. Kila unachogusa pia kimebarikiwa.

Unadhani habari njema kwa maskini ni ipi? Ni maisha mazuri ya utajiri na kuwa na kila kitu kwa wingi. Ndio maana aliwaambia "Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.” Mathayo 5:3

Maskini wakiupata Ufalme wa Mungu wanaondoka kwenye umaskini wao. Neno hilo hakuwaambia ili kuwasifia waendelee kuwa umaskini, hapana, aliwapa suluhisho la umaskini, ni kuupata ufalme wa Mungu.

Habari njema wenye dhambi ni kusamehewa na kuondolewa dhambi kwa njia ya imani kwa Yesu Kristo. Yaani, ukimuamini Kristo unaondolewa dhambi na kuwa mtakatifu na mwenye haki wa Mungu.

Habari njema kwa wagonjwa ni Bwana Yesu kuchukua magonjwa yao yote na kwamba hawapaswi kuumwa k**a wana imani kwa Yesu Kristo. Magonjwa yanakaa mbali.

Lakini kwa yule aliyekata tamaa kwa sababu ya magumu anayopitia, habari njema kwako ni hii, wanadamu hawawezi kila kitu lakini kwa Mungu mambo yote yanawezekana na atakusaidia.

Bwana Yesu ana mambo mema na mazuri kila siku kwa ajili yako, katika hali zote kuna habari njema kwa ajili yako; angalia ni habari njema gani anayo kwa ajili yako na kuhusu hitaji lako, angalia kwenye biblia.

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Mungu Wangu na Baba Yangu, Asante Kwa Kutupa Mwanao, Akaja Kutudhihirishia Upendo Wako Kwa Kutupa Habari Njema za Ufalme Wako, na Mapenzi Mema Juu ya Maisha Yetu. Hallelujah!

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Mathayo 4:23-24
23 Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu.

24 Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa hawawezi, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).

Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

03/10/2026

✍ Amekufa Lakini Ataishi
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Mathayo 9:18 SRUV
Alipokuwa akiwaambia hayo, tazama, akaja kiongozi mmoja, akamsujudia, akisema, Binti yangu sasa hivi amekufa; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Imani inajulikana pale tu ambapo utatamka neno. Ukisema una imani na hakuna unachotamka cha kudhihirisha kwamba kuna kitu una amini, hiyo haiwezi kuwa imani. Ili ujue mtu ana amini kitu gani, msikilize maneno yake.

Ukisoma neno letu la leo utaona kuna mtu kamuita Bwana Yesu kwenda kumfufua binti yake ambaye alikwisha kufa, na anasema hivi "Binti yangu sasa hivi amekufa." Unaweza ukasema huyu mtu hana imani, ila kuna neno moja alitamka likabadilisha kila kitu.

"lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi."

Alianza na neno "lakini," akiwa na maana kwamba hata k**a amekufa, bado inawezekana kuishi kwa hivyo "njoo uweke mkono juu yake." Imani haikatai kitu kilichotokea, ila ina uhakika wa hicho kitu kuwa k**a ambavyo anataka yeye.

Mathayo 9:23-25
23 Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo,

24 akawaambia, Ondokeni; kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana.

25 Lakini makutano walipoondoshwa, aliingia, akamshika mkono; yule kijana akasimama.

Unajua ni kwa nini haikuwa ngumu kwa Bwana Yesu kumfufua mtoto alikuwa amekufa tayari? Ni kwa sababu ya imani ya baba yake kwa njia ya maneno aliyotamka. Aliona amekufa ila akaamini kwamba anaweza kufufuka na Mungu akamfufua.

Usikatae kwamba unaumwa, lakini, amini kwamba kwa kupigwa kwake Yesu Kristo uliponywa. Usikatae kwamba hauna kitu fulani, lakini, amini kwamba Mungu wako atakujaza kwa wingi kila unachohitaji.

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Hakuna Jambo Lolote Linaloweza Kufa Kwenye Maisha Yangu Kwa Sababu Nipo na Kristo. Kwa Uweza wa Mungu Kila Kitu Ambacho Kimelala Kitaamka Tu. Hallelujah!

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Marko 5:41-42
41 Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka.

42 Mara akasimama yule kijana, akaenda; maana alikuwa amepata umri wa miaka kumi na miwili. Mara wakashangaa mshangao mkuu.

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).

Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

03/10/2026

✍ Umesamehewa Dhambi Zako
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 “Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, akiwa amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako. ”
Mathayo 9:2 SRUV
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Je! Wajua kwamba Bwana Yesu aliondoa kwanza dhambi, kisha ndipo magonjwa yaliponywa? K**a bado una amini kuwa wewe ni mwenye dhambi, huwezi kutoka kwenye magonjwa.

1 Petro 2:24
Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.

Jambo la kwanza lilikuwa ni kuondoa dhambi ambayo ndio chanzo cha magonjwa kuingia ulimwenguni. Pasipo uwepo wa dhambi, magonjwa hayawezi kupata nafasi kwenye mwili.

Sasa watu wanauliza kwa nini k**a Bwana Yesu alituponya magonjwa, tunaendelea kuumwa? Ndio alituponya, lakini aliondoa dhambi kwanza. Unapokea msamaha kwanza ndipo unapona.

Ni Wakristo wangapi wanakubali kwamba dhambi yao imeondolewa? Wengi sana wana imani kwamba wao ni wenye dhambi, magonjwa yanakaa kwenye dhambi. Pokea kwanza msamaha wa dhambi!

Unasumbuliwa sana magonjwa yasiyoisha? Una ugonjwa wa muda mrefu? Usiogope, amini umeondolewa dhambi na sasa wewe ni mtakatifu, kisha magonjwa yataondoka kwenye mwili wako.

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Nimeondolewa dhambi zangu zote, mimi ni mwenye haki wa Mungu katika Kristo. Nimepata ondoleo la dhambi, mimi sio mwenye dhambi tena bali mwenye haki na Mtakatifu. Hallelujah!

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
“Kwa maana rahisi ni lipi, ni kusema, Umesamehewa dhambi zako, au ni kusema, Ondoka, uende? Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Inuka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako. ” Mathayo 9:5-6 SRUV

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).

Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

02/10/2026

✍ Mmekuwa Waoga
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Mathayo 8:26
Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Bwana Yesu aliwakemea wanafunzi wake kwa sababu ya uoga waliokuwa nao, walipokutana na changamoto ya upepo na mawimbi baharini. Bwana Yesu alijuaje kwamba wana hofu?

Mathayo 8:23-25
23 Akapanda chomboni, wanafunzi wake wakamfuata.
24 Kukawa msukosuko mkuu baharini, hata chombo kikafunikizwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi.
25 Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia.

Wanafunzi wake walisema "tanaangamia," kudhihirisha jinsi gani walikuwa waoga. Mawimbi sio tatizo wala upepo haukuwa tatizo, hofu waliyokuwa wanayo ndio iliyokuwa tatizo.

Changamoto inapokuja haiji kukaa na wewe, inapita. Kitu pekee kitakachofanya isiondoke ni k**a wewe utakuwa na hofu. Haitaondoka, na itakuwa changamoto kubwa kuliko mwanzo.

Unapopata jambo gumu unapaswa kufanya nini? Cha kwanza kabisa ni kutulia, wala usikimbilie kwenye maombi kwanza mpaka upate utulivu, akili yako ikitulia unaweza ukaomba sasa.

Kwa nini usilimbilie kuomba kwanza? Ni kwa sababu utaomba vibaya, wanafunzi walipokuwa na hofu walisema "tunaangamia," asingekuwepo Bwana Yesu wangeangamia k**a walivyosema.

Ukifanya maombi wakati una hofu utaomba vibaya, tulia kwanza hofu ipungue au iishe kabisa; kisha fanya maombi na utaona mabadiliko kwa maana utaomba vizuri.

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Nakataa Kuwa Muoga Kwa Sababu Yoyote Ile, Nina Roho ya Nguvu Sio ya Woga. Hakuna Jaribu Linalokuja Ambalo Yesu Wangu Haliwezi, Atanisaidia Tu. Hallelujah!

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
“Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe. Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka? ” Mathayo 14:30-31 SRUV

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).

Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Website

Address


Arusha
23306

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ps. Emmanuel Cliff posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Subscribe

We will notify you when anything happens in Arusha.