Bongo Facts
Facts about Tanzania and other related Facts
22/09/2026
TANZIA 🕊️
Tumepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mama Fatma Karum, mjane wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, kilichotokea tarehe 21 Septemba 2026.
Mwenyezi Mungu amrehemu na ailaze roho yake mahali pema peponi. 🤲🏽
22/09/2026
🏦🇹🇿 Benki za Tanzania zang’ara duniani!
NMB Bank imepata nafasi ya 9, huku CRDB Bank ikishika nafasi ya 41 katika kundi la benki zenye mali kati ya dola bilioni 3–10 kwenye Forbes Top Performing Banks 2026.
Unaamini NMB au CRDB ndiyo bora zaidi?
21/09/2026
HERI YA SIKU YA AMANI DUNIANI SEPTEMBA 21
Haya ni mambo ya kufanya ili kulinda amani kupitia mitandao ya kijamii.
20/09/2026
🦓 Uhamaji wa wanyama Serengeti ni mojawapo ya matukio makubwa ya asili duniani.
Kila mwaka, zaidi ya nyumbu milioni moja, pamoja na pundamilia na swala, huhama kutafuta maji na malisho kati ya Tanzania na Kenya. 🌍
Ungependa kuuona maajabu haya siku moja?
19/09/2026
🏔️ JE, UNAJUA KILELE CHA JUU ZAIDI BARANI AFRIKA KIKO TANZANIA?
Mlima Kilimanjaro una urefu wa mita 5,895, na ndiyo kilele cha juu zaidi barani Afrika. 🇹🇿
Ungependa kuupanda siku moja?
17/09/2026
🇹🇿 JE, UNAJUA TANZANIA ILIPATA JINA LAKE LINI?
Tanzania haikuitwa Tanzania tangu mwanzo.
Tarehe 26 Aprili 1964, Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Jina Tanzania liliundwa kutokana na majina:
Tanganyika + Zanzibar = Tanzania
Baadaye, tarehe 29 Oktoba 1964, jina rasmi likawa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Muungano huu ni sehemu muhimu ya historia ya Tanzania na Afrika Mashariki. 🇹🇿
Swali: Ulijua kwamba jina Tanzania lilitokana na Tanganyika na Zanzibar?
Andika “Nilijua” au “Nimejifunza leo” kwenye maoni, kisha mtumie post hii mtu mwingine ajifunze pia.
Chanzo: Tanzania Embassy — Brief History
15/09/2026
Mwanza, Rock City
08/09/2026
🏙️🇹🇿 ARUSHA — JIJI LA KITALII.
Likiwa chini ya Mlima Meru, Arusha ni moja ya majiji muhimu Tanzania—likijivunia utalii na utamaduni wa kipekee. 🌍✨
Arusha si jiji tu, ni lango la Tanzania kwenda kwenye fursa za Afrika. 🇹🇿🔥
🚢🇹🇿 MV NEW MWANZA: FURSA KWA VIJANA
Teknolojia, mitandao na fursa za usafiri ni chachu ya biashara, ajira na maendeleo kwa vijana. Tuitumie mitandao kujenga fursa, kuunganisha jamii na kukuza uchumi—si kueneza taarifa za upotoshaji na kuvuruga amani.
🤝 Tuchague matumizi chanya. Tuchague maendeleo.
AmaniNiTrendYETU 🕊️
08/09/2026
🏟️🇹🇿 ARUSHA AFCON STADIUM YAENDELEA KUPAA! 🔥
Ujenzi wa Uwanja wa Arusha unaotarajiwa kuwa sehemu ya maandalizi ya AFCON 2027 unaendelea kwa kasi, huku miundombinu ya uwanja ikiendelea kujengwa kuelekea kukamilika. 🏗️⚽
🇹🇿 Tanzania inaendelea kujiandaa kwa AFCON 2027!
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Telephone
Website
Address
Dodoma
41101
Alerts
Be the first to know and let us send you an email when Bongo Facts posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.