Football Updates
✅Taarifa za soka la bongo
✅Tathmini za wachezaji
✅ Historia za wachezaji
✅Uchambuzi wa mechi za Yanga SC
05/08/2026
HII HAPA ORODHA YA VILABU BORA 10 AFRIKA kutoka CAF kwa timu zinazoshiriki CAF Champions League msimu ujao....
01. 🇿🇦 Mamelodi Sundowns — Alama 73
02. 🇹🇳 Espérance de Tunis — Alama 58
03. 🇲🇦 RS Berkane — Alama 57
04. 🇪🇬 Zamalek — Alama 49
05. 🇪🇬 Pyramids FC — Alama 48
06. 🇸🇩 Al Hilal — Alama 39
07. 🇹🇿 Simba Sports Club — Alqma 38
08. 🇹🇿 Young Africans SC — Alama 35
09. 🇦🇴 Petro de Luanda — Alama 27
10. 🇨🇮 ASEC Mimosas — Alama 24
Chama lako NAMBA NGAPI?!
05/08/2026
"Ninashindwa kwaeleewa" 🗣️ in Mchina's voice!! 😜
Kwahiyo Jaka Baller amesepa zake, ila ndugu yake Diarra bado yupo anadunda sana Chamazi...🔥
Kiutani utani panga linaweza kumkosa Sadio Kanoute...📌
By the way, ni mchezaji mzuri pia...
04/08/2026
Wakati kila mmoja akiandika na kusema lake kuhusiana na kiungo mshambuliaji wa Azam FC,Feisal Salum naomba nikumbushie jambo moja hapa;
Feisal amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na Azam FC...
Kiungo anahusishwa na vilabu vya Young Africans Sports Club na Simba SC Tanzania .
Niwakumbushe tu, mwaka jana wakati akiongeza mkataba, Feisal ndiye mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi NBC PL...
Baadhi ya terms tatu za moto zilikuwa hizi;
1. Azam walimpa Fei hela binafsi ya kusaini mkataba mpya (Sign on fee Tsh 800m cash).
2. Mshahara wa (Tsh 50m take home) kwa mwezi hii ni baada ya makato na kodi.
3. Ubalozi wa bidhaa/huduma zitolewazo na taasisi (Azam Pesa,Azam media nk.) ambapo kwa mwaka analipwa Tsh 200m.
Azam FC wali activate buyout clause yake kutoka $500,000 na mpaka $800,000 (billion 02 na chenji zake)
Fei anapiga pesa pale Azam FC 🔥
K**a timu yako ina ubavu wa kutoa Takriban Tsh. 2 Billion ruksa kufika mezani kwaajili ya kufanya biashara 😊
04/08/2026
Alex Iwobi: 🗣️
“Mechi yangu ya kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ilikuwa dhidi ya Barcelona yenye safu ya ushambuliaji ya MSN. Kila mtu aliogopa kumkaba Lionel Messi, hivyo nikajiambia, ‘Mimi nitamkaba.’
Mguso wake wa kwanza wa mpira ulinirusha kabisa. Ile chenga bado ipo YouTube hadi leo, na hata nilibadilisha mtindo wa nywele zangu ili watu wasinitambue k**a ni mimi ndio nilipigwa ile chenga.” 😆
La Pulga ameshindikana kitambo sana !!
04/08/2026
Young Africans Sports Club wamemtambulisha beki wao mpya, Farouk Komara raia wa Ivory Coast..
Msimu uliopita alifanya kazi na kocha wake ambaye pia amejiunga na Yanga, Manqoba Mngqithi wakiwa Golden Arrows ya Afrika Kusini..
Kwa uchache tu;
Komara ni pendekezo la kocha Manqoba.
Sifa kuu mbili zinazomfanya awe tofauti na mabeki wengi;
1. ball playing defender (anauwezo mzuri wa kupiga pass, habutui mipira ovyo)
2. Pressure absorber (Komara ana confidence ya kutosha kiasi cha kutokuwa na presha awapo uwanjani)
NEXT TIME, nitakuja na uchambuzi wa kiufundi nikielezea maeneo ambayo yuko imara na maeneo yenye madhaifu...
So far, huu ni usajili mzuri kwa Yanga SC.
Naamini Ibra Bacca, Mwamnyeto na Job wamepata mtu wa kuwachallenge baada ya kujimilikisha namba kwa misimu minne na zaidi...📌
03/08/2026
NDOTO INAYOTIMIA
Nassor Salum Nassor, dogo wa miaka 13 anayechezea timu ya vijana chini ya miaka 15 ya Azam FC.
Mwaka 2015 dogo huyu akiwa na miaka miwili, alipiga picha na mchezaji wa Azam FC, Serge Pascal Wawa.
Leo na yeye ni mchezaji wa Azam FC.
© Zaka Zakazi
03/08/2026
Kwenye moja ya interview zake, kocha mpya wa Young Africans Sports Club , Manqoba Mngqithi anasema yeye anapenda mchezaji anayekimbia maeneo mengi uwanjani..
Manqoba anasema, mikimbio anayoitaka yeye ni ile yenye maana (tactical runs) mfano, kukimbia kwaajili ya kumfanyia mpinzani pressing, kufungua nafasi ya kupasiwa, kuziba mianya nk. na si kukimbia tu ili mradi...
K**a ningeambiwa nitumie mfano hai wa aina ya wachezaji anaowahitaji Manqoba Mngqithi, basi ningekutajia Max Nzengeli...📌
Manqoba anataka timu yake iwe na work rate mithili ya ile ya Max Mpia...
Aina hii ya uchezaji inahitaji wachezaji wawe fit muda wote, ni approach hatari sana kwa wapinzani...
Ni aina ya uchezaji ambayo si tu kuamua temple ya mchezo bali pia humnyima mpinzani nafasi ya kujiuliza mara mbili awapo na mpira.
Kwenye clip za mazoezi ya Yanga, nilimsikia pia akisisitiza wachezaji wake wahakikishe wana maintain ile temple yao wakiwa kwenye pressing...
Manqoba Mngqithi is cooking 📌
31/07/2026
Bus la kifahari la simba aina ya Irizar limeharibika njiani wakielekea karatu kwenye uzinduzi wa jezi yao mpya
Uzuri walikuwa wamesafiri na fundi wao.
©Katunzi blog
😂😂 Eboh! mambo ya VITU USED haya...
Tayari Irizar ya mnyama Simba SC Tanzania imetaga huko..
Narudia tena, Irizar IMETAGA HUKO 😂
31/07/2026
Katika kujiandaa na msimu mpya, kikosi cha Young Africans Sports Club kimecheza mechi ya kirafiki leo pale Avic Town dhidi ya timu ya Magereza Dar Es Salaam...
Yanga wameibuka na ushindi wa magoli 7 - 2.
Magoli ya Yanga yamefungwa na;
⚽️ Chadrack Boka🎯 Maxi Nzengeli
⚽️ Albert Kangwanda 🎯 Cheikh Touré
⚽️ Depu
⚽️ Edmund John
⚽️ Depu 🎯 Allan Okello
⚽️ Allan Okello
⚽️ Casemiro 🎯Mpemba D
29/07/2026
Tangu nilipomtizama kwenye mechi 03 za mwanzo, nilishapitisha uwezo wake ✅
Niliandika baada ya kuondoka kwa Fiston Mayele, sasa Young Africans Sports Club wamepata mshambuliaji mwingine tishio mbele ya lango..
Laurindo Dilson Aurelio Mario Depu ni miongoni mwa washambuliaji wenye ufanisi mkubwa wa kubadilisha nafasi kuwa magoli...
K**a si majeraha aliyopata msimu uliopita, huenda angemaliza kinara kwenye orodha ya wafungaji...
Msimu uliopita amefunga jumla ya mabao 14 🔥
09 - NBC Premier League
02 - CAF Champions League
03 - CRDB Federation Cup
Ikumbukwe, Depu ni ingizo la dirisha dogo msimu uliopita..📌
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Address
Dodoma