Manispaa ya Lindi

Manispaa ya Lindi

Share

This is the official page of Lindi Municipal Council

Photos from Manispaa ya Lindi's post 20/09/2026

MANISPAA YA LINDI YAONGEZA TAHADHARI KUKABILIANA NA MVUA ZA EL NINO

📌Weka Akiba ya Chakula

Manispaa ya Lindi imeendelea na zoezi la usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali, likiwemo kusafisha mitaro na mifereji pamoja na kuondoa taka, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Nino.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha njia za maji zinakuwa wazi na kupunguza hatari ya mafuriko. Wananchi pia wametakiwa kushirikiana na Manispaa kwa kuepuka kutupa taka ovyo, hususan kwenye mitaro na mifereji.

Aidha, wananchi wametakiwa kujiandaa kwa kuweka akiba ya vyakula na mahitaji muhimu, pamoja na kuzingatia usalama kwa kukaa katika maeneo yasiyo hatarishi ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa mvua hizo.

Photos from Manispaa ya Lindi's post 19/09/2026

DR KIRUSWA AWATAKA WACHIMBAJI LINDI KUONGEZA THAMANI YA MADINI

Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven L. Kiruswa, amewataka wachimbaji wadogo mkoani Lindi kuunganisha nguvu na kuwekeza katika viwanda vya uchakataji wa madini ili kuongeza thamani ya madini yanayozalishwa na kuongeza fursa za ajira na biashara.

Dkt. Kiruswa ametoa kauli hiyo leo, Septemba 19, 2026, wakati akifunga Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Lindi, akieleza kuwa Serikali ina mpango wa kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata madini ya nikeli ndani ya mkoa huo.

Aidha, amezitaka taasisi na mashirika yaliyoshiriki maonesho hayo kuanza maandalizi mapema kwa ajili ya maonesho ya mwaka 2027, akisema hatua hiyo itasaidia kuyaimarisha zaidi na kufungua fursa nyingi kwa wananchi.

Sambamba na hilo amesisitiza kuwa maonesho hayo yanaendelea kuwa jukwaa la kuwaunganisha Serikali, wachimbaji, wawekezaji, wafanyabiashara na taasisi za fedha.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Adam Malima, amesema sekta ya madini imeendelea kukua na maonesho hayo yamekuwa muhimu katika kuitangaza Lindi na kuunganisha wadau na fursa za uwekezaji.

Amesema Serikali ya Mkoa itaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha madini yanachochea ajira, biashara na maendeleo ya wananchi.

19/09/2026

Viwanja vya madini Ruangwa
Wizara ya Madini
Mkoa Wa Lindi

18/09/2026
18/09/2026

Wananchi mnakaribishwa kujifunza namna ya kutengeneza bidhaa mbalimbali na kupata ujuzi wa kuongeza thamani ya bidhaa kupitia ubunifu na ujasiriamali.

📍 Viwanja vya Madini, Ruangwa
Usikose fursa hii ya kujifunza na kukuza ujuzi wako

Photos from Manispaa ya Lindi's post 18/09/2026

PROF. SHEMDOE AITAKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI KUHARAKISHA UPATIKANAJI WA HATI YA ARDHI YA KAMPAS YA UDSM LINDI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, ameiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa hati ya umiliki wa ardhi kwa ajili ya Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Lindi.

Prof. Shemdoe ametoa agizo hilo Septemba 16, 2026, Ruangwa mkoani Lindi, katika kikao kazi kilichohusisha viongozi wa Serikali na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili kampasi hiyo.

Amemtaka Bw. Mnwele kulishughulikia suala hilo na kutoa mrejesho wa utekelezaji, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba, alilolitoa wakati wa ziara yake mkoani Lindi.

Katika hatua nyingine, Prof. Shemdoe ameiagiza TARURA Mkoa wa Lindi kukamilisha maandalizi ya ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 1.5, itakayounganisha Kampasi ya UDSM Lindi na barabara kuu ya Lindi.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Adam Kighoma Malima, pamoja na viongozi na wataalamu kutoka Serikali na UDSM, akiwemo Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Bernadeta Killian.

prof RIZIKI SILAS SHEMDOE
Adam Malima Kam
Mkoa Wa Lindi
Juma Mnwele

Photos from Manispaa ya Lindi's post 17/09/2026

📌Mining Expo 2026, Ruangwa

Kupitia Madini Expo 2026, wananchi wanaendelea kupata elimu kuhusu fursa zinazotokana na sekta ya madini na namna zinavyoweza kuchochea shughuli za kiuchumi, kuongeza ajira na kukuza pato la taifa.

Picha hizi zinamuonesha Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Adam Malima, akitembelea Banda la Manispaa ya Lindi na kuzungumza na wajasiriamali kuhusu fursa za kiuchumi zinazotokana na maonesho hayo.

Sambamba na hilo, viongozi wamepatiwa elimu kuhusu afua za lishe, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha jamii kuzingatia afya na lishe bora kwa ajili ya kuwa na nguvu kazi yenye tija.

Wizara ya Madini
Adam Malima Kam
Zuwena Jiri
Juma Mnwele
Hassan Tanzanite Ngoma
DUNIA HADAA
Mohamedi Hamisi Mohamedi

17/09/2026

Je, wewe umejifunza nini kupitia elimu hii ya Lishe Bora?, Mining Expo utajifunza mengi. Karibu Ruangwa Katika Banda la Manispaa ya Lind ufahamu jinsi ya kupangilia afya yako.

Photos from Manispaa ya Lindi's post 17/09/2026

FURSA ZA MADINI ZALENGA KUONGEZA MANUFAA KWA WANANCHI LINDI

Na Dawla Muni- Mining Expo 2026 Ruangwa

Fursa za uwekezaji katika sekta ya madini zimejadiliwa mkoani Lindi, huku matumizi ya taarifa sahihi za madini na teknolojia yakisisitizwa k**a njia ya kuongeza uwekezaji na manufaa ya rasilimali hizo kwa wananchi.

Hayo yameelezwa leo, Septemba 17, 2026, katika Kongamano la Fursa za Biashara na Uwekezaji lililofanyika Viwanja vya Madini Ruangwa, likiwakutanisha wafanyabiashara, wawekezaji na wadau mbalimbali.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Adam Kighoma Malima, amesema ramani za madini ni muhimu katika kutambua maeneo yenye uwezekano wa kuwa na rasilimali hizo na kuwawezesha wawekezaji kufanya maamuzi sahihi.

Amesema kuunganisha mitaji, teknolojia na utaalamu na fursa zilizopo mkoani humo kunaweza kusaidia kuendeleza shughuli za uchimbaji na kuongeza manufaa ya madini kwa wananchi.

Wadau pia wamejadili matumizi ya teknolojia za kisasa na upatikanaji wa taarifa za madini, kwa lengo la kukuza uwekezaji na kuhakikisha rasilimali hizo zinawanufaisha zaidi wananchi wa Lindi.

Wizara ya Madini
Adam Malima Kam
Zuwena Jiri
Mkoa Wa Lindi
Juma Mnwele

Photos from Manispaa ya Lindi's post 17/09/2026

📌Lishe Bora Msingi Wa Maendeleo ya Kiuchumi

Na Dawla Muni- Mining Expo 2026 Ruangwa

Wananchi wamejitokeza kwa hamasa kupata elimu ya afya na lishe mapema leo katika Banda la Manispaa ya Lindi, kwenye Maonesho ya Madini – Mining Expo Ruangwa 2026.

Pamoja na uwekezaji katika sekta ya madini, afya ni uwekezaji muhimu katika kujenga jamii yenye afya na yenye uwezo wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na maendeleo ya taifa.

Kujitokeza kwa wadau kupata elimu ya lishe ni hatua muhimu katika kuimarisha afya na ustawi wa jamii.

Karibu Banda la Manispaa ya Lindi! Karibu Mining Expo Ruangwa 2026.

Want your organization to be the top-listed Government Service in Lindi?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


Lindi
255

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Manispaa ya Lindi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Subscribe

We will notify you when anything happens in Lindi.