fmmanyara

fmmanyara

Share

Fm Manyara Radio ni Redio Bora inayopatikana wilayani Babati Mkoani Manyara.

FM Manyara inawafikia zaidi ya wasikilizaji Milioni Mbili kupitia masafa ya 92.3 katika mikoa ya Manyara,Arusha, Singida na Dodoma
Tunazalisha vipindi bora kila siku
Kwere Street

11/09/2026

Aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ufana wilayani Babati mkoani Manyara Paulo Stephen Mapunda, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Babati, akikabiliwa na jumla ya makosa 12, yanayohusiana na kughushi nyaraka za malipo na matumizi ya fedha za shule.

Kesi hiyo imesikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Babati, huku upande wa Serikali ukiwakilishwa na Mawakili wa Serikali kutoka TAKUKURU, Neema Gembe na Davis Masumbu ambao wamesema Msh*takiwa alitenda makosa hayo kati ya December 12 2024 Hadi February 28 2025.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa mahakamani hapo Mapunda anatuhumiwa kufanya makosa ikiwemo kughushi nyaraka na hati za malipo, pamoja na kutumia nyaraka hizo katika mchakato wa matumizi ya fedha kiasi cha shilingi milioni tano na elfu themanini na tano (5,085,000) kupitia akaunti ya shule kwa matumizi binafsi.

Kesi hiyo imeahirishwa Hadi September 12 na Msh*takiwa amekana kesi inayomkabili na amepata dhamana baada ya kukidhi vigezo vya kuwa na wadhamini 2 ambao wamesaini hati ya dhamana million 10.

10/09/2026

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imeagiza Mkuu wa Majeshi (CDF), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kufika mahakamani kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.

Uamuzi huo umetolewa na Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru leo, Septemba 10, 2026.

Uamuzi huo umetokana na maombi yaliyowasilishwa mahakamani yakitaka viongozi hao kutoa ushahidi katika kesi hiyo.

Photos from fmmanyara's post 07/09/2026

Shirika la umeme Tanzania TANESCO mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na jeshi la polisi limewakamata watu watatu wa kitongoji Cha Ndoroboni kijiji cha Kiru six kwa tuhuma za kuunganishiwa umeme kinyume na Sheria .

Afisa uhusiano TANESCO mkoa wa Manyara Samwel Mandar pamoja na msimamizi wa kitengo Cha udhibiti mapato TANESCO mkoa wa Manyara Maisha Mchuruza amesema watu hao wameunganishiwa umeme bila kufuata utaratibu wa Tanesco.

Baadhi ya watuhumiwa ambao wameunganishiwa umeme wamesema waliunganishiwa na mtu Mmoja ambae alijifanya mfanyakazi wa Tanesco na kuwaambia watoe pesa ili waunganishiwe umeme.

Mwenyekiti wa kitongoji cha ndoroboni kijiji cha Kiru six Ramadhani Juma amesema hana taarifa za wananchi hao kuunganshiwa umeme, ambapo amewataka wananchi wake kufuata hatua zote za kuunganishiwa umeme.

07/09/2026

Mume wa Rais Samia afariki dunia

Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, ametangaza kifo cha Hafidh Ameir Hassan, ambaye ni mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Taarifa ya Makamu wa Rais kwa vyombo vya habari, imesema Ameir amefariki dunia leo Septemba 7,2026 katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Mzena Zanzibar, alipokuwa akipatiwa matibabu ya moyo.

Taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika visiwani Zanzibar na ratiba ya maziko itatolewa.

07/09/2026

Mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Hafidh Ameir, amefariki dunia.

Taarifa za kifo cha Hafidh Ameir, zimetangazwa na Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi kupitia vyombo vya habari.

Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa Jina lake lihimidiwe

03/09/2026

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Queen Sendiga, amekabidhiwa rasmi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Adam Malima, katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Malima amesema ataendelea kumpa ushirikiano Sendiga, ikiwemo kutoa ufafanuzi kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wake.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Queen Sendiga, amewaomba watumishi wa mkoa huo kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake na kuhakikisha shughuli za maendeleo zinaendelea kwa ufanisi.

Aidha, Sendiga amefurahishwa na uwepo wa wawakilishi wa waandishi wa habari kutoka mkoani Manyara, ambao walifunga safari hadi Morogoro kushuhudia makabidhiano hayo.

Photos from fmmanyara's post 02/09/2026

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za bidhaa za mafuta ya Petroli zitakazoanza kutumika kuanzia Jumatano, Septemba 2, 2026 saa 6:01 usiku.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano ya kwanza ya mwezi Septemba 2026, bei za Mafuta nchini zimeshuka kwa Shilingi 102 kwa lita na Petrol na Shilingi 101 kwa lita ya Dizeli. Hii ni kutokana na hatua mbalimbali ambazo Serikali imezichukua ili kuwa na bei himilivu za Mafuta hapa nchini

Kwa Dar es Salaam, bei ya rejareja kwa lita moja itakuwa Sh3,796 kwa petroli, Sh3,877 kwa dizeli na Sh3,713 kwa mafuta ya taa.

Mkoani Tanga, Petroli itauzwa kwa Sh3,872, Dizeli Sh3,953 na Mafuta ya taa Sh3,789 kwa lita, wakati huo Mtwara, bei ya petroli itakuwa Sh3,909, dizeli Sh3,990 na mafuta ya taa Sh3,825 kwa lita.

Aidha, EWURA imewataka Wafanyabiashara wa Mafuta kuuza bidhaa hizo kwa bei zisizozidi viwango vilivyotangazwa, huku ikisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara atakayekiuka agizo hilo.

01/09/2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, am ya kuwasalimu na kuzungumza na wananchi wa eneo la Mbuyuni wilayani Moshi, wakati alipowasili mkoani humo kwa ziara maalumu.

Wananchi mbalimbali wamefurika katika eneo hilo kumpokea na kumsikiliza Makamu wa Rais Deogratius Ndejembi ambapo yupo mkoani kilimanjaro kwa ziara maalumu ya kwenda kuwaona ndugu zake ambao wanaishi katika eneo hilo.

Ni ziara ya kwanza nje ya Dodoma tangu aapishwe kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Kisimachahabari

01/09/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Leo ameshiriki sherehe za uapisho wa Hakainde Hichilema kuwa Rais wa Jamhuri ya Zambia.

Rais Samia ametumia fursa hiyo kupitia mtandao ya kijamii kumpongeza Rais Hichilema kwa kuaminiwa tena na wananchi wa Zambia.

"Ninawahakikishia ndugu zetu wa Zambia kuwa Tanzania itaendelea kuthamini na kuimarisha uhusiano wetu wa kidugu, wa kihistoria na kimkakati, kwa manufaa ya nchi zetu mbili." Rais Samia

Want your business to be the top-listed Media Company in Manyara?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Address


Kwere, Babati
Manyara

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when fmmanyara posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Subscribe

We will notify you when anything happens in Manyara.