Dc-Mbinga

Dc-Mbinga

Share

Tovuti rasmi ya Ofisi ya
Mkuu wa Wilaya ya mbinga.

Photos from Dc-Mbinga's post 07/08/2026

Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe. Kisare Makori, leo tarehe 07 Agosti 2026, ametembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga katika Maonesho ya Wakulima ya Nanenane, yanayoendelea jijini Mbeya.
‎
‎Mhe. Makori amepata fursa ya kujionea vipando mbalimbali vya mazao, teknolojia za kilimo pamoja na bidhaa zenye thamani zinazozalishwa na wajasiriamali kutoka Wilaya ya Mbinga.

Photos from Dc-Mbinga's post 13/07/2026

Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe. Kisare Makori, leo Julai 13, 2026, ametembelea na kukagua banda la Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga pamoja na mabanda yanayowakilisha Mkoa wa Ruvuma katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere, jijini Dar es Salaam.
‎
‎Mhe. Makori amepata fursa ya kujionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiriamali wa Wilaya ya Mbinga na Mkoa wa Ruvuma, zikiwemo bidhaa zilizoongezwa thamani kupitia ubunifu na teknolojia.

Photos from Dc-Mbinga's post 10/06/2026

‎Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe.Kisare Makori akizungumuza wakati wa ufunguzi wa semina ya wadau wa Maji Halmashauri ya Mbinga Mji leo tarehe 10/6/2026.
‎
‎Semina hiyo imeandaliwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbinga Mjini ( MBIUWASA).

Photos from Dc-Mbinga's post 18/05/2026

‎Mkuu wa Wilaya ya Mbinga,Mhe.Kisare Makori, leo Mei 18,2026 amekabidhi Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe.Kapenjama Ndile.
‎
‎Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru 2026 baina ya Halmashauri ya Mji wa Mbinga na Manispaa ya Songea yamefanyika katika Kijiji cha Likuyufusi.
‎
‎“Tanzania ni yetu sote, Tushikamane kwa pamoja kuleta Maendeleo.”

Photos from Dc-Mbinga's post 17/05/2026

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Ndugu. Wazo Mwang’onda, amegawa bure majiko ya gesi pamoja na mkaa wa nishati safi kwa makundi maalum katika eneo la Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mbinga (FDC), Halmashauri ya Mji Mbinga ili kuunga mkono dhamira ya dhati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan Katika kuendelea kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ili kutunza na kulinda mazingira dhidi ya ukataji ovyo wa miti kwa ajili ya matumizi ya Kuni na Mkaa badala yake tutumie Nishati mbadala

“Tanzania ni yetu sote, Tushikamane kwa pamoja kuleta Maendeleo “

Photos from Dc-Mbinga's post 17/05/2026

Wakazi wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wanatarajiwa kunufaika kiuchumi kupitia mradi wa shamba la kahawa aina ya Arabica uliokaguliwa leo Mei 17 na Mwenge wa Uhuru.

Mradi huo wenye ukubwa wa hekari 20 umegharimu shilingi milioni 337 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2022, huku ukiwa tayari umezalisha tani 1.5 za kahawa katika msimu wa 2025/2026.

Akikagua mradi huo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka huu, Wazo Mwang’onda, amesema uwepo wa shamba hilo ni fursa muhimu kwa vijana kujipatia ajira, kuongeza vipato pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Mkoa wa Ruvuma kupitia sekta ya kilimo cha kahawa.

Mbali na kuongeza uzalishaji wa kahawa, mradi huo umeelezwa kutoa ajira kwa vijana na wanawake zaidi ya 30 pamoja na kuongeza mapato ya Halmashauri ya Mji Mbinga kupitia shughuli za biashara.

17/05/2026

Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe.Kisare Makori akiwa sambamba na viongozi Mbio za Mwenge Kitaifa 2026 wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga.

Photos from Dc-Mbinga's post 17/05/2026

Mwenge wa Uhuru leo tarehe 17, Mei 2026, Umekagua Mradi wa Kikundi cha Bodaboda cha Winner kilichopo kata ya Mbambi, Halmashauri ya Mji wa Mbinga.
‎
‎Kikundi hicho ni matokeo ya dhamira ya dhati ya serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwafikia vijana kupitia Mikopo ya asilimia 10% inayotolewa na Halmashauri kwa ajili ya Vijana na Makundi maalumu.
‎
‎"Tanzania ni yetu sote, Tushikamane kwa Pamoja kuleta Maendeleo"

Photos from Dc-Mbinga's post 17/05/2026

Mwenge wa Uhuru leo tarehe 17 Mei 2026 Umekagua Huduma za Afya zinazotolewa na Majengo ya Wagonjwa wa Nje (OPD), Maabara na Upasuaji katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Mbinga.
‎
‎"Tanzania ni yetu sote, Tushikamane kwa Pamoja kuleta Maendeleo"
‎

Photos from Dc-Mbinga's post 17/05/2026

‎Mwenge wa Uhuru leo tarehe 17 Mei 2026 Umekagua Huduma za Afya zinazotolewa na Majengo ya Wagonjwa wa Nje (OPD), Maabara na Upasuaji katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Mbinga.
‎
‎"Tanzania ni yetu sote, Tushikamane kwa Pamoja kuleta Maendeleo"

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Mbinga?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address


Mbinga

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dc-Mbinga posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Subscribe

We will notify you when anything happens in Mbinga.