Efatha Ministry_Mikese..Moro
Religion organisation
10/12/2025
Hakika hii isikupite wewe unaesoma ujumbe huu AMEN
30/05/2024
NENO LA SIKU
Na, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira- Kanisa la Efatha
TAREHE: 30/05/2024
SOMO: TAMANI KUJIFUNZA NENO LA MUNGU
Wewe ni UTUKUFU wa Mungu hivyo tamani kuwa UTUKUFU wake, lakini ili kufikia hapo kuna gharama unayotakiwa kulipa, hata Yesu alitukuka sana lakini alilipia gharama. Yeremia, Eliya, Elisha, Daudi, Solomoni n.k, wote walipitia maumivu na changamoto ili wafike hapo walipofika, leo hii tunasoma habari zao na kutiwa moyo lakini wao walikubali kulipa gharama.
Baadhi ya wakristo siku hizi wanapenda kusikia Unabii tu lakini hawataki kulipia gharama ya huo Unabii, kimsingi ni kuwa Unabii haupo ili kukufikisha kule unakotaka kufika bali utafika kule unakotaka kufika kutokana na utendaji wako.
Wana wa Israeli ili waifikie nchi ya Ahadi ambayo Mungu aliwaahidi, haikuwa rahisi, walikaa jangwani kwa muda wa miaka 40 walipitia vikwazo vya kila aina japo kuwa ulikuwa ni Unabii. Walipoingia nchi ya Ahadi walikutana na mapambano na vita lakini ulikuwa ni Unabii.
Watu wengi siku hizi hawapendi kujifunza au kusikia Neno la Mungu litakalowasaidia wao kutenda sawa na Mapenzi ya Mungu bali wanapenda kusikia Unabii tu, hivyo kuwasababisha kuhangaika huku na kule ili kutafuta Unabii. Unapaswa kujua kuwa Unabii upo ili kukutia moyo na kukuwezesha wewe kusonga mbele lakini si kukupa stahiki yako, Imani yako ndiyo itakufanya upokee stahiki yako kutoka kwa Mungu, kwa sababu Imani yako itakupa Tumaini la kungoja kile unachokiamini mpaka kitakapotokea.
Mwana wa Mungu, tamani kujifunza Neno la Mungu litakalokupa Imani na Tumaini la kungoja kile Mungu amekuahidi na si kusikia Unabii ambao hata ukichelewa kutimia kwako utakusababisha wewe kuhangaika huku na kule.
19/05/2024
NGUVU YA MAOMBI
Yakobo 4:2
[2]Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!
Katika hiki kipindi cha kufunga na kuomba tunapaswa twende mbele zake tukiwa na hoja (maombi). Lakini katika kuomba kwetu ni lazima tuombe katika njia impendezayo yeye na siyo kutazama kiu ya nafsi zetu
Mathayo 6:9-10
[9]Basi ninyi salini hivi;
Baba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe,
Ufalme wako uje,
[10]Mapenzi yako yatimizwe,
hapa duniani k**a huko mbinguni.
Maombi yetu ni lazima yawe na upatanisho na mapenzi ya Mungu ili yakapate kibali na kujibiwa sawasawa na mapenzi yake
18/02/2024
MAAMUZI YA MTU KUMILIKI
Na MCH: PAULO DOTTO
Ili mtu aweze kumiliki ni lazima azikane njia zake zote potofu na kufata maagizo ya Mungu maana yeye ndiye mpaji
Danieli 3:28
Nebukadreza akanena, akasema, Na ahimidiwe Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego; aliyemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake waliomtumaini, wakaligeuza neno la mfalme, na kujitoa miili yao ili wasimtumikie mungu mwingine, wala kumwabudu, ila Mungu wao wenyewe.
👉Ili kuweza kumiliki, mtu anahitaji kuingia ghalama kubwa ya vile alivyonavyo
🤲Mathayo 19:15-22
[15]Mtu Aliyekuwa Tajiri
[16]Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele?
[17]Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri.
[18]Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo,
[19]Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako k**a nafsi yako.
[20]Yule kijana akamwambia, Haya yote nimeyashika; nimepungukiwa na nini tena?
[21]Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.
[22]Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
11/02/2024
SOMO: TUMAINI
Na Mch: Paul Dotto
Tarehe: 11/02/2024
TUMAINI
Ili watu wawe na urafiki wa kweli lazma wawe na upendo, imani na tumaini ndani yao
1wakorintho13 Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
Mtu akiwa na upendo, tumaini na imani lazma atampendeza Mungu.
Mtu akiwa na hivi vitu vitatu lazma atatembea na neno la ushindi siku zote kwamaana msingi wa haya yote ni NENO
Waebrania 11:1
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
14/01/2024
Dady
MAISHA YA TOBA NI MSINGI WA UBAADAE WAKO
Na Mt: BICHILA
KANISA LA EFATHA MIKESE
Makundi matatu
1. Ni lile linalotafuta pesa na kutumia (halina malengo)
2. Ni lile linalotafuta pesa kwa malengo
watu waliopo katika kundi hili huwa na sifa ya ubahili ili kutimiza malengo
3. Ni lile linalotamani kupata pesa lakini hawazitafuti
watu wanaopatikana katika kundi hili hudondokea katika wimbi la umaskini.
ili kuepukana na haya yote tunahitaji akili ya Kiungu ili kuweza kupata mafanikio yaliyokusudiwa(hasa kundi la 1 na 3)
Zaburi 51: 1-4
katika zaburi hii tunamuona mt: Daudi ambaye alitambua kuwa kwa hali ya uovu uliokuw umemzunguka kamwe asingempendeza Mungu ndipo alipoamua kuingia katika toba ili kujitakasa na kutafuta upatanisho na Mungu(Mfalme Daudi aliishi maisha ya toba)
Hata katika biblia wapo waliofeli kwa kukosa maisha ya toba k**a vile SAULI
Katika maisha tunayoishi, TOBA ni silaha itakayotupa upatanisho wetu na BABA yetu wa mbinguni
17/07/2022
IBADA YA JUMAPILI KANISA LA EFATHA MIKESE, 17/07/2022
Na Mt: Mhaiki, E
NGUVU YA KUTOA
VIPINGAMIZI/VIKWAZO KATIKA KUTOA
katika kutoa au kumtolea Mungu, vipo vizuizi au vikwazo vinavyoinuka ili kukwamisha!
Shetani anajua nguvu iliyomo ndani ya utoaji itokayo kwa Mungu hivyo huinua vikwazo/vizuizi ili kuzuilia
👉ubinafsi wa mtu mwnenyewe
👉uchoyo wa mtu
👉kibuli cha mtu/mwanadamu
👉Wivu wa mtu binafsi
Mwanzo 22:1-12
marko 12:42-44
🙏Tunajifunza katika kutoa kuna utii k**a ilivyokuwa kwa mama mjane na pia Ibrahimu
🙏Kwenye kutoa kuna maumivu
🙏 kwenye kutoa kunahitaji utayari
🙏Pia kwenye kutoa kuna mateso
🙏 Kuna kusikia sauti ya Mungu
17/07/2022
IBADA YA JUMAPILI KANISA LA EFATHA MIKESE, 17 JULY 2022
NGUVU YA KUTOA
Na Mt: Mhaiki, E
👉NGUVU ni msukumo ulio ndani ya mtu unaomuwezesha kufanya jambo
👉KUTOA ni kukabidhi au kumpa mtu kitu
umiliki wa kitu flani kutoka kwa mtu mmoja ili kiwe cha mtu mwingne mfano pesa, gari, vazi, nk
Matendo ya mitume 20:35
👂Katika mambo yote nimewaonesha ya kuwa kwakushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu jinsi alivyosema mwenyewe, ni heri kutoa kuliko kupokea
☝☝☝☝☝☝☝☝☝☝
Katika andiko hili tunajifunza kuwa utamaduni wa kutoa ulikuwepo tangu zamani. Mababu zetu walitoa vitu vya thamani kubwa k**a sadaka kwa miungu yao ili aweze kuvipokea na kuviridhia. Sisi tunayo neema kwamba Mungu tunayemtolea ni Mungu wa kweli ambaye alikuwepo tangu enzi na enzi
KWA NINI TUNATOA
🙇Tunatoa ili kujipatanisha na Mungu
🙇Tunatoa ili kujitambulisha kwake
🙇Ili kujionesha kwa Mungu
🙇Tunatoa ili kuiga tabia yake BWANA
🙇 Tunatoa ili kumpendeza Mungu wetu
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Morogoro
Alerts
Be the first to know and let us send you an email when Efatha Ministry_Mikese..Moro posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.