Fivara

Fivara

Share

Hip-Hop/Rap artist from Tanzania, East Africa. page for Tanzanian Hip-Hop artist, Songwriter and Producer - Fivara.

20/09/2026

Usikose Jumamosi ijayo Nafasi Art Space Mikocheni 🔥🔥🔥

17/09/2026

No cap, kwanza hii imeandikwa kwa CAPS LOCK.

17/09/2026

KIPINDI WOTE TUPO.
Nimekua nikiona challenge ya picha za zamani lakini hii ya familia imenigusa zaidi kwa sababu nikiziona nakumbuka “kipindi wote tupo”.
Challenge ya picha za zamani (haswa ya muonekano wako miaka ya 1980) imeshika hatamu, watu wengi wamepost picha zao kwa msaada wa akili mnemba (AI) wakapata mandhari na muktadha wa miaka hiyo. Ukiachana na challenge hiyo niliona pia baadhi ya watu wakitengeneza na kuweka picha za zamani za kifamilia.

Nilipoziona picha hizo likaja wazo “Kipindi wote tupo” kwa maana nikiziangalia picha hizo naona ni kipindi ambacho familia nyingi watu wote/wengi walikuwepo. Ni kipindi ambacho tulikua hatujapoteza ndugu zetu wa karibu aidha wazazi, kaka, dada, wadogo, shangazi, mjomba, babu, bibi nk. Ni kipindi ambacho marafiki zetu walikuwepo. Kipindi ambacho furaha ilikua imetawala na hatujui kuhusu kifo. Tulijiuliza watu wakifa wanaenda wapi, hatukujua. Hata watu walipokufa baadae tulipouliza tulijibiwa wameenda mbali na maneno mengine ya kutupumbaza.

Kwangu picha hizi ni zaidi ya challenge, zinanisafirisha kihisia na kunipeleka wakati huo tupo wote. Kipindi kaka yangu sio marehemu wala baba yangu sio marehemu. Kipindi tunajumuika pamoja kula chakula cha jioni. Harufu ya wali maharage au ugali nyama au makande na mara nyingine kiepe (zege la nyumbani) vinanijia kichwani. Kuna aina ya muziki nausikia kichwani aidha ni nyimbo za injili kv Rose Muhando, Upendo Nkone au ni za Rhumba, au Msondo Ngoma kina Tx Moshi na nyinginezo.
Picha k**a hiyo hapo juu inanikumbusha vibe ka sikukuu ambalo hivi sasa halipo tena. Inanikumbusha sauti mbalimbali nilizokua nikizisikia nyumbani tofauti na miaka ya sasa hata k**a kuna sauti lakini ukimya ni mwingi. Inanikumbusha kipindi ambacho nilifurahia moments bila kujua kwamba nitazikumbuka moments hizo. Inanikumbusha kipindi ambacho sina madeni, siwazi kuhusu projects, kipindi ambacho sina wasiwasi, hofu, wala mawazo ya kesho yangu. Kilikua ni kipindi ambacho niliishi wakati uliopo. Kilikua ni KIPINDI AMBACHO WOTE TUPO!

16/09/2026
15/09/2026

Tukutane tarehe 26 mwezi huu (Jumamosi ya wiki ijayo) Nafasi Art Space Mikocheni kwenye Wikiendi LIVE festival 🔥🔥🔥

10/09/2026

Ikiwa leo ni World Su***de Prevention Day ebu weka namba yako tukupigie tukujulie hali, tukutie moyo ma hata kukupongeza.

Hii haijalishi uko sawa au hauko sawa, una mawazo au hauna, we weka namba tuongee na k**a kuna lolote tutashirikishana.

Unaweza pia kumpigia mtu yoyote atakaeweka namba lakini pia wapigie ndugu, rafiki na jamaa zako wa muda mrefu uwasalimie, uwajulie hali nk.

10/09/2026

To whoever is reading this and quietly fighting a battle nobody knows about — please hold on.

I know life can become heavy. Sometimes the pain feels bigger than your strength, and the future can feel impossible to imagine. But this moment is not the whole story of your life.

Please don’t face it alone. Talk to someone you trust. Reach out. Let somebody sit with you through the difficult days. Asking for help is not weakness — it is courage.

And if someone around you has been distant, unusually quiet, or seems to be struggling, check on them. Listen. Don’t judge. Sometimes a simple “How are you really doing?” can open a door someone desperately needs.

Your story is still being written. There are conversations you haven’t had, places you haven’t seen, people you haven’t met, and moments you haven’t lived yet. YOU MATTER, YOU ARE NOT ALONE.

— Jordan “Fivara” Zabron
Mental Health Advocate

10/09/2026

Bila sales kutoa capital au elimu ya ughavi bro lakini najikuta tu na faida.

Mko tayari kwa Hii Sio Freestyle 5?

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Mwanza?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Address


Mwanza

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Fivara posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Subscribe

We will notify you when anything happens in Mwanza.