Ibrahim Jeremiah
GOD fearing man,Politician,Businessman with a lovely heart and best ideas to develop Tanzania,Africa
01/05/2026
UKIAMBWA “HIVI VINA PESA UTAKUWA TAJIRI” — JIHADHARI.
UNAWEZA KUISHI MAISHA YOTE UKISUBIRI MAFANIKIO YASIYOKUJA.
Hizi ni sehemu wengi wanapoteza muda na pesa wakidhani ni fursa....
lakini ukweli wake huu hapa:
1. Forex
Watu wanaona screenshots za profit na motivation, wanaingia kwa pupa.
Kwa Tanzania, wanaopata pesa consistent kwenye forex wengi wao sio traders — ni wauzaji wa kozi, signals, au mentorship.
Trader halisi hawana makelele utaishia mikononi mwa wauza kozi..
Wewe unaingia bila skill → unakuwa chanzo cha pesa kwa broker na kwa anayekufundisha.
⸻
2. Crypto
Wanakuambia “nunua mapema utapata faida mara 10.
Lakini nani anakuuzia hiyo coin? Ni mtu aliyenunua zamani.
Hii game ina waliofanikiwa wachache sana mi sijui hata mmoja aliyefakiwa kwenye maisha halisi zaidi ya status na waliochelewa wanabeba hasara.
Wengi wanaingia kwa hype, wanatoka wakiwa wamepoteza pesa na muda.
⸻
3. Betting
Hii sio fursa, ni biashara yao dhidi yako.
Mfumo umejengwa wewe ushindwe taratibu, sio ushinde.
Unashinda kidogo → unarudisha yote + zaidi.
Mtu akikwambia utegemee betting anakupoteza...
Mwisho unakuwa addicted, sio tajiri.
⸻
4. Network Marketing (MLM reality)
Unaambiwa “leta watu, utapata pesa ukiwa umekaa.”
Unaambiwa utakua tajiri na kutengeneza mamilioni kwa muda wa ziada...
Ukweli hii ni biashara k**a biashara nyingine na kuna kampuni kaa nazo mbali kabisaa.
Ingawa ukipata kampuni yenye product nzuri, ukapata mentor mzuri na ukawa na skills za kuuza utatengeneza pesa ila Sio kila mtu ana skill ya kuuza na kujenga team wengi wanaishia kukata tamaa
⸻
5. “Online Hustles” zisizo na mfumo (mfano: kutegemea apps random, surveys, kuangalia ads)
Unaambiwa “tengeneza pesa ukiwa nyumbani bila mtaji.”
Utapoteza muda tu hapa, unauza muda wako kwa senti.
Hizi sio biashara ni distraction zinazokufanya ujione uko bize wakati haujengi chochote. Waachie wavivu waangalie matangazo walipe buku
⸻
6. Kuagiza Bidhaa China bila mfumo.
Hii inaonekana strong sana na ndio wengi wanaingia sasa hivi.
Aisee hapa ukiingia kichwa kichwa hasa kuagizia wengine utaishia kwenye madeni au mahak**ani
Hata kuagiza vyako Wengi wanaingia sababu umeona “watu wanauza” Hujui nani atanunua kwako, Huna brand, huna audience, huna strategy
Matokeo yake Unakuwa na mzigo ndani, pesa imekwama, unaanza kuuza kwa hasara au kuomba wateja.
Biashara sio kuagiza bidhaa ni kuuza bidhaa.
⸻
7. Utengenezaji content.
Unapost sana, unapata likes, followers wanaongezeka.
Unakuwa maarufu kidogo… lakini maskini bado.
Utaishia kujichetua k**a hakuna bidhaa, hakuna huduma, hakuna target audience, hakuna mfumo wa mauzo.
⸻
Msinirushie mawe niliotaja fursa zenu....
Najua....
Vitu hivi vinaweza kuingiza pesa — NDIO
Lakini sio kwa mtu anayeingia k**a mtazamaji
Pattern ipo wazi:
✅Wanaopata pesa → wanauza system, elimu, au wana skill ya juu
✅Wanaopoteza pesa → wanakuja k**a watazamaji wa mafanikio ya wengine
Ukiona kitu kinaonekana rahisi sana kupata pesa, jua wewe ndio bidhaa.
Kwa sababu
* Kuna anayekufundisha → analipwa
* Kuna broker/platform → analipwa
* Kuna aliyekuuzia idea → ameshalipwa
Wewe bado unatafuta “utapataje.”...
FURSA GANI KWENYE HIZI HUTAKI HATA KUISIKIA?
02/04/2026
Nafasi ya kazi
Tunatafuta binti ambaye ni Muhasibu/Internal Auditor
Ofisi zetu zipo Posta, Dar es Salaam Tanzania
Kwa mawasiliano piga
0622 896789
05/02/2026
Wewe ni Mbegu
Ukitupwa ardhini hautakufa,
Utaota na kustawi vizuri!
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Songea
Alerts
Be the first to know and let us send you an email when Ibrahim Jeremiah posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.