DNPC DONGOBESH

DNPC DONGOBESH

Share

Blessed Valley Church
Neno | Maombi | Kuhubiri
DONGOBESH, Manyara

30/09/2026

Bwana Yesu asifiwe tunapenda kuwaalika katika Kongamano kubwa la kuvunja siku tatu za madhabahu za shetani

Ni hapa DNPC DONGOBESH

Usipange kukosa mtu wa Mungu

Photos from DNPC DONGOBESH's post 27/09/2026

Askofu Mathew J Tsuut na Askofu Somi Severua Kaaya wakiwa katika studio za shalom radio baada ya uchaguzi wa DNPC kitaifa ambapo walikuwa na viongozi wengine na Watumishi wa Mungu wengine

Photos from DNPC DONGOBESH's post 27/09/2026

Ibadani leo hakika ilikua ya Baraka sana!

24/09/2026

Askofu mkuu wa kanisa la DNPC Taifa Rev.Mathew Jacob Tsuut amesema uongozi mpya wa kanisa utaendeleza dhima ya umisheni kwa mataifa yote k**a lilivyo jina la kanisa.

"Utumishi wa Mungu ni mzigo unao hitaji kuufikisha kwa namna ya kipekee"Rev.Mathew Jacob Tsuut

Photos from DNPC DONGOBESH's post 31/07/2026

Kanisa la DNPC limeweka wakfu marekebisho ya katiba yake k**a hatua muhimu ya kuimarisha utendaji wa kanisa, kukuza uwajibikaji, weledi na ufanisi katika utumishi.

Akizungumza katika tukio hilo, Katibu Mkuu wa Kanisa la DNPC, Mathew Jacob, amesema marekebisho hayo yanalenga kuendana na mahitaji ya wakati, kuwajengea viongozi uwezo wa kulitumikia kanisa kwa ufanisi, pamoja na kutoa nafasi kubwa zaidi kwa vijana kushiriki katika uongozi na kuchangia maendeleo ya kanisa na taifa kwa ujumla.

“Kizazi cha leo ni viongozi wa kesho.”

20/07/2026

Hatuwezi kufikia malengo bila kuomba | Rev Mathew Jacob

Photos from DNPC DONGOBESH's post 19/07/2026

REV MATHEW JACOB
MAMBO MANNE YESU ALIFANYA ALIPOKUA DUNIANI

KUOMBA
Yesu aliweka kipaumbele cha kwanza kwenye mawasiliano na Baba. Alitenga muda wa faragha na kukesha akiomba.
• Maandiko ya Rejea:
• Luka 6:12 (Alikesha usiku kucha akimuomba Mungu)
• Mathayo 26:40-41 (Kukesha na kuomba ili usiingie majaribuni)
• Luka 18:1-2 (Mfano wa kuomba sikuzote bila kukata tamaa)

ALIFUNDISHA
Alishiriki maarifa na kanuni za Ufalme wa Mungu kwa kina ili kuwapa watu ufahamu na hekima ya maisha.
• Mithali 11:2

YESU ALIHUBIRI
Alitangaza Habari Njema ya ukombozi na kuwalingania watu watubu ili kuingia katika Ufalme wa Mungu.
• Mathayo 10:5-8

YESU ALIPONYA WAGONJWA
Hakuhubiri kwa maneno tu, bali alionyesha upendo wa Mungu kwa vitendo kwa kuponya wagonjwa na kufanya miujiza.

Huduma ya Yesu ilikuwa kamilifu—Ilihusisha roho (kuomba/kuhubiri), akili (kufundisha), na mwili (kuponya). Sisi k**a wafuasi wake tunapaswa kufuata nyayo hizi.

13/07/2026

Tunavyopata nafasi, Tusichoke kutenda mema | Ev Zawadiel

Photos from DNPC DONGOBESH's post 12/07/2026

REV MATHEW JACOB
KUNYENYEKEA CHINI YA MKONO WA MUNGU ULIOHODARI
1.Mkono wa Mungu Unaoa na Kusikia
ISAYA 59:1-2
Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hatA lisiweze kusikia;

2. Mkono wa Mungu Ndio Muumba na Hakuna Linaloshindikana
YEREMIA 32:17
Aa! Bwana MUNGU, tazama, wewe umeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa; hapana neno lililo gumu usiloliweza;

3. Mkono wa Mungu Unatenda Makuu na Unatoa Uzima
ZABURI 118:16-17
Mkono wa kuume wa BWANA umetukuzwa; Mkono wa kuume wa BWANA hutenda makuu.

Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya BWANA.

4.Wajibu Wetu: Kunyenyekea Ili Kuinuliwa
1 PETRO 5:6
Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;
-
Mkono wa Mungu una nguvu ya kuokoa, kuumba, na kutenda makuu. Hakuna gumu linaloshindikana chini ya mkono huo. Wajibu wetu mkuu ili kuuona ushindi huu ni **kunyenyekea** chini yake, naye kwa wakati wake atatunua.

Photos from DNPC DONGOBESH's post 21/06/2026

EV ZAWADIEL MATHEW
KADRI TUNAVYOWEZA KUPATA NAFASI, TUSICHOKE KUTENDA MEMA.
Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema..." Wagalatia 6:9-10

Maisha ya Mkristo ni maisha ya upendo kwa vitendo. Wakati mwingine tunachoka au kukata tamaa tunapoona wema wetu hauthaminiwi, lakini Neno la Mungu linatukumbusha mambo haya 3 muhimu leo:

1.Nafasi hazidumu milele
Tumia kila fursa unayoipata leo kuwa baraka kwa mtu mwingine. Usisubiri kesho, maana huenda fursa hiyo isiwepo tena (Mhubiri 9:10).

2.Wema wako ni Injili tosha
Watu wengi watasoma tabia na matendo yako kabla ya kusoma Biblia. Matendo mema ni nuru inayomtukuza Baba wa mbinguni (Mathayo 5:16).

3.Mavuno ni ya hakika (Kuwa na subira)
K**a mkulima anavyosubiri mazao, usikate tamaa k**a huoni matokeo sasa hivi. Mungu si dhalimu hata asahau upendo unaouonyesha (Waebrania 6:10).

Mambo unayoweza kufanya leo
• Kumsaidia au kumwombea mwenye uhitaji.
• Kuwafariji wenye huzuni na kusamehe waliokukosea.
• Kuweka hazina mbinguni badala ya kutafuta sifa za wanadamu (Mathayo 6:20).

Neno la Leo: Tenda mema kwa moyo safi. Mungu anaona kila unachofanya kwa siri, na atakulipa kwa wakati wake!

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Mapumulo?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Website

Address


DONGOBESH
Mapumulo

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when DNPC DONGOBESH posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Subscribe

We will notify you when anything happens in Mapumulo.